Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Kifo cha Suluhu; (i) Kinaya (ii) Barua

      

Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Kifo cha Suluhu;
(i) Kinaya
(ii) Barua

  

Answers


Francis
i. Kinaya.
Abigael anasema kuwa babake anamtegemea kwa kila kitu. Ni kinyume baba kumtegemea mwanawe, tena mwana anayesoma. Ndiye anatarajiwa kumsaidia mwanawe.
Abigael anasema kuwa mkewe Suluhu hana amani kutokana na mali ya mumewe. Ni ajabu mali ya mumewe kumkosesha amani badala ya kumfariji.
Ni kinaya kuwa Suluhu anatafuta njia ya kumwangamiza mkewe, ambaye anafanya kila awezalo kumvumilia. Ndiye analea watoto wao peke yake. Anamtunzia siri zake nzito. Ajabu ni kuwa Abigael, anayemfanya kuwazia haya ananuia kujinufaisha kutoka kwake, hata yuko radhi kumwua.
Bi. Suluhu analazimika kumwandikia mumewe barua kumpasha ujumbe wake. Ni kinaya kuwa hana muda wa kuwasiliana na mume wake.
Suluhu anamkodishia kimada wake nyumba mjini ili mkewe asijue, ila kimada mwenyewe anamweleza mkewe kila kitu.
Ni kinaya kwa Suluhu kumwambia mkewe watoto ni wake peke yake. Wanaume hutarajiwa kuonea fahari watoto zaidi ya wake zao. Isitoshe, Bi. Suluhu anasema kuwa anajua mumewe atafurahi kuwa mwanao wa kwanza amekamilisha masomo ya msingi, ambayo Suluhu mwenyewe hajachangia!
Bi. Suluhu anasema kuwa kifo chake kitahesabiwa haki. Ajabu ni kuwa amepitia mengi mikononi mwa mumewe hadi kuhiari kufa. Kwa hakika, kifo chake hakiwezi kuwa haki. badala ya ukweli huu kumtia machungu zaidi kumwua, unamfanya kughairi nia na kumwacha hai.

ii. Barua
Bi. Suluhu anamwandikia mumewe barua kumweleza uchungu anaomsababishia.
Mumewe ametengana naye na hapati fursa ya kuzungumza naye. Barua hii inaanguka mikononi mwa Abigael.
Inadhihirisha kero anazopitia Bi. Suluhu na ukatili wa mumewe, ikiwemo kumwua mamake Abigael. Inamwonyesha Abigael anavyomsababishia mateso na hata hatari anayojiweka kuhusiana na Suluhu aliyebeba nakama. Inamfunza umuhimu wa utu na kumfanya kughairi nia ya kumwua Suluhu.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 09:25


Next: “Mabadiliko ni mambo ya lazima katika jamii,” thibitisha kauli hii katika hadithi ya Kifo cha Suluhu.
Previous: Fafanua masuala yafuatayo katika hadithi, Ahadi ni Deni; (i) nafasi ya mwanamke katika jamii (ii) Familia na Malezi

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions