Fafanua masuala yafuatayo katika hadithi, Ahadi ni Deni; (i) nafasi ya mwanamke katika jamii (ii) Familia na Malezi

      

Fafanua masuala yafuatayo katika hadithi, Ahadi ni Deni;
(i) nafasi ya mwanamke katika jamii
(ii) Familia na Malezi

  

Answers


Francis
(i) nafasi ya mwanamke katika jamii
Jamii hii inaonekana kumkandamiza mwanamke, japo kuna matumaini ya maisha bora kwake. Mwanamke anawasilishwa kuwa msomi. Fadhumo anapelekwa na babake mjini kuandaliwa kujiunga na shule ya upili, anayoacha baada ya kufiwa na wazazi. Hata hivyo, anarejea masomoni miaka sita baadaye na kupata ufanisi mkubwa.
Mwanamke anachukuliwa kama chombo cha starehe. Jamaa ya babake Fadhumo anataka kujistarehesha na Fadhumo kimahaba ili kuwasaidia nduguze kupata elimu, lakini anakataa.
Mwanamke pia anachukuliwa kuwa mtumishi wa nyumbani. Watu wanamwambia Adan kuwa hafai kumwacha Fadhumo aendelee na masomo wala kazi bali anafaa kukaa nyumbani ili atunze boma. Mamake Fadhumo hahusishwi katika kumwandaa kujiunga na shule. Ni baba anayeandamana naye mjini.
Mwanamke pia anaonekana kama kiumbe dhaifu asiyestahili makuu. Mjombake Adan anamwambia kuwa hafai kumwacha mkewe azidi kusoma, kwamba amesoma vya kutosha. Anaona kuwa akizidi kusioma atakuwa mjeuri. Mjombake Fadhumo anakubali kumlipia kakake lakini si yeye.

(ii) Familia na Malezi.
Fadhumo anajaliwa familia inayomwezesha kukua na kusoma. Babake anampeleka mjini kumnunulia vitu vya kujiunga na shule ya upili. Pia, binamu wa babake anakubali kuishi naye wakati wa likizo ya mihula ya kwanza miwili.
Wazazi wake wanapofariki, analazimika kuacha shule kuwakidhi nduguze kama mwanambee wa familia. Mjombake anafadhili elimu ya kakake. Jamaa wa babake anamtaka kuwa kimada ili awakimu lakini anakataa.
Fadhumo anapata familia yake mwenyewe anapoolewa na Adan. Anamwoa ili aweze kumsaidia kukidhi mahitaji ya wanuna zake. Wanajaliwa wana watatu na hata Fadhumo yuko tayari kupata zaidi. Anawalea wanawe kwa staha na kumfanya Adan ayaone malezi kuwa mepesi kama kanda la usufi.
Mjombake Adan anamwita anapohisi kama mambo hayaendi sawa. Anamtaka kumkomesha mkewe kusoma. Mjomba huyu ndiye amemlea Adan baada ya babake kufariki. Hivyo, Adan anamheshimu na kumsikiza, licha ya kuwa hayuko tayari kutekeleza matakwa yake wakati huu.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 09:28


Next: Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Kifo cha Suluhu; (i) Kinaya (ii) Barua
Previous: Je, anwani, Toba ya Kalia inafaa? Eleza.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions