Je, anwani, Toba ya Kalia inafaa? Eleza.

      

Je, anwani, Toba ya Kalia inafaa? Eleza.

  

Answers


Francis
‘Toba’ ni majuto yanayotokana na kutenda maovu. Hivyo basi, mada hii inarejelea majuto ya Kalia kutokana na maovu aliyotenda. Ndilo tukio kuu katika hadithi hii.
Siri anampa Jack ujumbe kuwa amewaalika pamoja na wazazi wake katika kipindi cha Nyumbani ni Nyumbani kwenye runinga ya Kikwetu. Anamwambia kwamba ana ujumbe muhimu ambao angependa ulimwengu ujue, lakini asimwambie babake. Sababu ni
kuwa unahusu uovu wa Kalia.
Siri anapoulizwa kuhusu safari ya mafanikio yake, Kalia anaenda msalani kumjulisha kuwa kuna sehemu ya historia hiyo isiyofaa kusikika na yeyote. Hii ni sehemu aliyompoka Jack haki. Hataki kukiri makosa yake na kuomba toba, hadi muda unapofika.
Siri anasimulia Jack alivyoshinda katika mashindano na kutwaa fursa ya kusomea Uchina, lakini Kalia akampoka nafasi hiyo na kumwekea mwanawe, Siri, aliye huko wakati huu. Anajuta sana kwa hilo, na anamwomba Jack msamaha, na pia kwa ajili ya wazazi wake. Jack anawasamehe.
Kalia anaomba msamaha pia kutokana na kitendo chake. Kuonyesha toba yake ni ya dhati, anaahidi kuyashughulikia masomo ya Jack hadi atakapo.
Kando na hayo, matendo ya Kalia yanastahili toba, kwani anamchukulia Jack nafasi hiyo, licha ya kuwa na uwezo wa kumsomesha Siri bila msaada. Anayepokwa nafasi hiyo ni yatima! Si hayo tu, Kalia aliahidi kumsomesha hadi atakapo baada ya wazazi wake kuaga.
Jack anapoanzisha biashara ya viatu, anaanza kuimarika na hapo wazazi wa Siri wanaanza kudai nusu ya faida yake, eti ni zawadi ya malezi. Hata hivyo, Jack anawasamehe wala hana kinyongo. Anaikubali toba ya Kalia.
Kitendo cha Siri kwa Kalia ni toba. Anamwanika kwenye runinga ya Kikwetu kutokana na matendo yake ya awali. Kisa cha Jack kinamwuma kiasi cha kutovumilia na kuamua kuuambia ulimwengu. Hawezi kuvumilia zaidi.

francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 10:46


Next: Fafanua masuala yafuatayo katika hadithi, Ahadi ni Deni; (i) nafasi ya mwanamke katika jamii (ii) Familia na Malezi
Previous: Fafanua kwa kina masuala ibuka yafuatayo katika hadithi ya Toba ya Kalia; (i) Elimu (ii) Teknolojia na mawasiliano

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions