Fafanua kwa kina masuala ibuka yafuatayo katika hadithi ya Toba ya Kalia; (i) Elimu (ii) Teknolojia na mawasiliano

      

Fafanua kwa kina masuala ibuka yafuatayo katika hadithi ya Toba ya Kalia;
(i) Elimu
(ii) Teknolojia na mawasiliano

  

Answers


Francis
i. Elimu.
Jack na Siri wanasoma katika shule moja ya upili ambayo ni maarufu nchini. Wanatamatisha elimu ya kidato cha nne pamoja, na Jack anampiku Siri kwa pointi tano.
Inawawezesha kushiriki katika shindano linaloandaliwa na wahandisi kutoka Uchina na kuibuka katika nafasi tatu za kwanza.
Mashindano hayo yanamwezesha Siri kupata fursa ya kuendeleza elimu yake Uchina, japo ni Jack anayestahili nafasi hiyo. Jack anaandaa kazi ya kupigiwa mfano na hata fomyula zake zinaingizwa kwenye vitabu, japo kwa jina la Siri.
Jack pia akiwa Uchina anaendeleza elimu ya lugha ya Kiswahili kwa wakazi wa huko, na anasema kwamba baadhi yao wanapata umilisi hata kuliko wazungumzaji wa nchi yake ya nyumbani. Anaimarisha ujuzi wake wa lugha kwa kusoma riwaya mbili, tamthilia mbili na diwani ya amashairi kila mwezi.
Jack anapokamilisha masomo yake ya shule ya upili, anakosa namna ya kuendelea kwa kuwa wazazi wake waliaga. Anaanza biashara ya kuuza nguo lakini baada ya Siri kuanika matendo ya Kalia hewani, hali inabadilika. Anapata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu kwa ufadhili wa Kalia.
Kando na hayo, Bi. Mshewa pia ameelika hadi kuwa mwalimu wa Kiswahili, sawa na Bi. Gatoni, mtangazaji na mwendeshaji wa kipindi cha Nyumbani ni Nyumbani katika runinga ya Kikwetu.

ii. Teknolojia na Mawasiliano.
Hadithi inadhihirisha maendeleo ya teknohama katika jamii. Jack anapokea simu kutoka kwa Kalia, kumweleza kuhusu mwaliko wa Siri katika mahojiano kwenye runinga ya Kikwetu. Wakiwa njiani, Jack anakumbuka baruapepe aliyotumiwa na Siri kumfahamisha kuwa kuna siri alitaka kusema.
Tunaambiwa kwamba Siri huwasiliana na wzazi wake kupitia skype, na Jack ndiye huwaunganishia mitambo kuhakikisha mawasiliano yanafaulu vizuri. Wanapatana naye vyema akiwa Uchina.
Ukumbi wa mahojiano unadhihirisha hali ya teknolojia na mawasiliano kwa uwazi. Jack anaketi karibu na mtangazaji, huku mkabala mwa mtangazaji mna kiwambo kikubwa kama ukuta. Hapa ndipo picha ya Siri inatokea wakati wa mahojiano na wanaendesha shughuli nzima bila matatizo. Kalia anapohisi hatari ya Siri kutaja yasiyofaa, anaelekea msalani kumkumbusha kuhusu hayo. Hata hivyo, mawasiliano hayakamiliki kwani simu ya Siri haipatikani kwa wakati huo.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 10:56


Next: Je, anwani, Toba ya Kalia inafaa? Eleza.
Previous: Taasubi ya Kiume na migogoro ni baadhi ya masuala makuu katika hadithi, Nipe Nafasi. Jadili.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions