Taasubi ya Kiume na migogoro ni baadhi ya masuala makuu katika hadithi, Nipe Nafasi. Jadili.

      

Taasubi ya Kiume na migogoro ni baadhi ya masuala makuu katika hadithi, Nipe Nafasi. Jadili.

  

Answers


Francis
1. Taasubi ya Kiume/ Ubabedume
Kazili anapata fununu kwamba mumewe ana mke mwingine migodini. Hata hivyo, inaaminika kwamba mwanamume ana uhuru wa kuwa na wake wengi atakavyo, lakini mke mwema hafai kulalamika. Mume mwenyewe hamtumii pesa na anapozituma kupitia kwa mamake hazimfikii mkewe.
Mama Kazili anapofika kwa Matweba, analaumiwa kwa kuondoka nyumbani bila ruhusa ya mumewe, wala hata kumwambia.
Wanaona huko kama kumdharau mumewe. Anapotaka ajira, wanasema kuwa hapaswi kuifanya bila idhini kutoka kwa mumewe.
Kazili anaeleza jinsi wanaume wanavyojitukuza kwa kusingizia Biblia, inayosema wanawake wawe wanyenyekevu kwa waume zao. Wanatakiwa kuwaomba waume zao ruhusa kufanya kila kitu, hata kutembelea familia na marafiki zao.
Wanaume wanaposikia maneno ya Kazili, wanabaki kinywawazi kwa kutoamini. Wanadai kwamba anafaa kurudi kwa wazazi wake Swaziland kwa kuwakosea heshima. Wanawake wazee wanaamini kuwa amewakosea heshima wanaume. Wamepandishwa wadhifa sana kiasi cha kuruhusiwa kuwadhulumu wanawake watakavyo.
Wanaume pia ndio wanaopatiwa wadhifa wa kusuluhisha matatizo ya familia. Ni wao tu wanaoruhusiwa kwenda kwenye kraal kufanya maamuzi kuhusiana na masuala ya familia. Wanadai kwamba Mungu aliwapa wadhifa wa uongozi.
Maamuzi yanayotolewa kwenye kraal yanachukuliwa kuwa sheria wala hayafai kubadilishwa. Matweba anapotoa habari za yale waliyoamua, watu wanaanza kufumukana kwani wanaamini kwamba hiyo ndiyo sheria wala haifai kupingwa.
Msimulizi anaeleza tukio la kijijini Habelo, baada ya mwanamke mmoja kumwambia mumewe ni mzembe kandamnasi. Wanaume wanaanza kukutana kuelezana jinsi mwanamke huyo alivyokosa heshima. Anatoweka kijijini na watu wanafikiri aliamriwa kurudi kwao, hadi mbwa wanapofukua mwili wake kondeni mwao. Mumewe alimuua na kumzika.

2. Migogoro
Msimulizi anashuhudia migogoro kati ya wazazi wake. Babake anafanya kazi migodini Afrika Kusini, hali mamake anaishi kijijini Habelo. Ana mke mwingine huko, na pia hamtumii mama pesa, na anapotuma hazimfikii. Japo anajua hili, anadai kwamba ameshindwa kuishi na mke anayeshinda kulalamika. Mama anaamua kuondoka kwenda kwa jamaa ya babake.
Mama na wanawe wanapofika kwa Matweba, mgogoro unazuka. Mama analaumiwa kwa kuondoka bila ruhusa, lakini anadai kwamba hangekaa tu wanawe wakihangaika, na pia alijua hangeruhusiwa.
Anaeleza kwamba yuko tayari hata kutafuta kazi, kinyume na taratibu.
Kazili pia anazua mgogoro miongoni mwa wanwake. Wale wazee wanaona kwamba amekosa heshima kwa wanaume, lakini wake wachanga wanahongera juhudi zake.
Maamuzi ya wanaume kwenye kraal yanawazulia mgogoro mwingine na Kazili. Hakubaliani na maamuzi yao wala hayuko tayari kuyafuata. Wanajiandaa kufumukana lakini anasema maoni yake kwa ujasiri.
Anaanguka na kuwalazimu kummwagia maji. Mwishoni mwa mwaka, amekuwa mwalimu wa shule ya msingi bila ruhusa kutoka kwa yeyote.
Msimulizi anaeleza mgogoro uliotukia Habelo miaka miwili awali, baada ya mwanamke mmoja kumwita mumewe mzembe kandamnasi. Wanaume wanasemezana jinsi alivyokosa maadili kwa wanaume.
Hatimaye anatoweka, na baadaye kubainika mumewe alimuua na kumzika kondeni mwao.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 11:15


Next: Fafanua kwa kina masuala ibuka yafuatayo katika hadithi ya Toba ya Kalia; (i) Elimu (ii) Teknolojia na mawasiliano
Previous: Mwandishi wa hadithi, Nipe Nafasi ameshughulikia vipi suala la ’ utamaduni na mabadiliko’

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions