Huku ukitolea mifano, eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Nilitamani; (i) Kinaya (ii) Taharuki (iii) Taswira

      

Huku ukitolea mifano, eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Nilitamani;
(i) Kinaya
(ii) Taharuki
(iii) Taswira

  

Answers


Francis
i. Kinaya
Tumaini anasema kwamba Nina alimkirimia kama mama yake kwa kila kitu. Hata hivyo, anaamua kuondoka kwake, japo hana pa kuishi na kuishi kwa rafiki yake Jenifa. Ni ajabu kuwa anachoka kufadhiliwa hali hana hanani.
Tumaini anasadiki kwamba alimwonea gere Nina. Haya ni licha ya roho ya utu ya Nina, ambaye anamkidhia haja zake zote. Tumaini anapopata hela kutoka kwa Nina, anaamua kwenda kudanganya moyo Coco Beach. Ananunua kaukau za mihogo na soda ya pepsi na kuketi akitazama bahari. Anavinjari kama mwenye vyake hali anateseka.
Tumaini anasema kwamba hapendi kusema na wageni lakini Romeo anaonekana kuwa mwungwana. Tunagundua baadaye kwamba si mwungwana hata kidogo. Sura yake pia ni kinyume cha uhalisia wake.
Tumaini anaiona Jumamosi hii anayokutana na Romeo kuwa ya fanaka maishani mwake. Hata hivyo, ni matata zaidi ambayo inamletea mikononi mwa Romeo.

ii. Taharuki
Mwanzoni, tunabaki kujiuliza maswali kadhaa kuhusu msimulizi. Ni nani, yuko wapi na anasumbuka kwa nini. Haya yanatanzuka taratibu masimulizi yanavyozidi.
Tumaini anatuambia kuwa ana mwana, Radhi, ambaye amemwacha kwa bibi yake, Farida. Hatujajuzwa kuhusu wazazi wake, na mazingira aliyopata huyo mtoto, kwani ni wazi kuwa hana mume.
Jenifa ni rafiki ya Tumaini ambaye anamkidhia mahitaji yake ya kimsingi. Hatujaelezwa zaidi kumhusu, hususan usuli wake wala kazi anayofanya.
Tumaini anafikiri kwamba Romeo ni Mkenya, lakini anagundua baadaye kwamba asili yake ni Zanzibar. Romeo awali anamwambia kwamba alimwona Westlands, jijini Nairobi. Hatujui iwapo ni ukweli aliwahi kumwona au amejua ni Mkenya tu kwa mbinu nyingine. Tumaini mwenyewe anakana japo tunajua ni Mkenya.
Tumaini anapogundua nia ya Romeo, anafaulu kuponyoka kutoka garini mwake na kuyoyomea vichakani. Hatujui hatima yake ni gani.tunabaki na maswali tele. Je, atajua vipi njia ya kurudi Kigamboni? Ataendelea kusaka ajira au atahiari kurudi Kenya? Tuseme hatarudi nyumbani, Jenifa atachukua hatua gani? Na je, Romeo aliyemtoroka atamfuata au labda kumnasa kwa mbinu ya giza? Tamaa ya Tumaini itafika kikomo au ataendelea tu kutamani? Na maswali mengi mengine.

iii. Taswira
Taswira ya mume wa Nina; …alivyokuwa na mume mzuri, mrefu kiasi, si mweusi si mweupe. Tabasamu nzuri iliyoficha pua ya kubabatana. Asiyekonda wala kuwa mnene. Miguu iliyojaa vizuri na kulainishwa na weusi wa malaika…
Taswira ya Tumaini pale Coco Beach; ufuoni nikanunua kaukau za muhogo na soda ya pepsi. Nikatandaza pareo yangu, nikakaa nikiangalia bahari… ile bahari iliashiria maisha yasiyokuwa na mwisho…
Taswira ya Romeo; Alikuwa wa asili ya Kiarabu. Mweupe, macho yake ya wastani meupe kama theluji ila malegevu. Uso wenye umbo la embe dodo, kidevu kimenyolewa vizuri utadhani kimechongwa na kuacha uso kung’aa. Nywele za singa zinanukia udi hasa. Mwili wote unanukia riha ibura ya uturi. Mikono imechongeka vizuri kwa misuli ya wastani. Kifua nacho ni cha ngao. Usiseme maguu manene yaliyoketi vizuri kwenye kaptura lake la buluu. Pale Romeo anapompeleka Tumaini; …Romeo aliegesha gari, akaanza kunionyesha majumba ya kifahari kwenye ufuo wa bahari, penye miti iliyoshika rangi yake ya kijani
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 11:34


Next: Mwandishi wa hadithi, Nipe Nafasi ameshughulikia vipi suala la ’ utamaduni na mabadiliko’
Previous: Je, anwani Pupa inafaa? Fafanua.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions