Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Umaskini na usherati ni baadhi ya mambo ambayo hudidimisha maendeleo. Thibitisha kauli hii ilivyotumika katika hadithi, Pupa.

      

Umaskini na usherati ni baadhi ya mambo ambayo hudidimisha maendeleo. Thibitisha kauli hii ilivyotumika katika hadithi, Pupa.

  

Answers


Francis
1. Umaskini
Mwakuona amezaliwa katika familia ya kimaskini. Wanaishi katika mtaa duni wenye nyumba zilizojengwa karibu kwa mabati
makuukuu, udongo, mahema makuukuu na hata katoni. Zinajiinamia na kuwa na thamani ya chini kama wanaoishi huko. Wakazi wanazaa watoto wengi, huku wakiwa na imani mmoja akifanikiwa, atatoa familia katika umaskini.
Mwakuona anaona mengi katika maisha yake. Ana nguo moja ambayo anafua na kungoja ikauke avae. Wazazi wake wanataabika
kuwalisha kila siku. Yeye na ndugu zakewakubwa wanalazimika kukwangura mabaki na ukoko ili wachanga wapate angaa tonge.
Wanapatwa na utapiamlo na unyafuzi. Nywele zinageuka hudhurungi na miguu kufanya matege. Miguu isiyojua viatu inakaukiana na kujaa tekenya.
Bi. Mtego anatumia umaskini wa Mwakuona kama chambo cha kumnasia. Anamweleza kuhusu kampuni ambayo inafadhili safari za vijana kwenda ng’ambo na kuwafadhilia masomo. Hali hii inamtia Mwakuona hamu ya maisha na kuondoka umaskini. Anakubali rai yake. Anaona akilini mwake maisha mazuri, vyakula vya kifahari na nguo nzuri. Anaazimia hata kuhamisha familia
yake hadi mtaa wa kifahari na kuelimisha nduguze.
Umaskini pia unakatiza juhudi na tumaini la wazazi wa Mwakuona kumpata. Hawajampigisha picha awali kutokana na hali yao.
Isitoshe, hawana hela za kutosha kuwasaidia polisi kumsaka au kama wanavyosema wao, ‘kuwatilia gari mafuta’ . Wanakata tamaa ya kumwona mwanawe. Mwakuona anapotoroka Chenga-ways, anashangaa iwapo watamkubali. Aliondoka maskini wa mali, sasa ni maskini wa kila kitu.

2. Uasherati.
Bi. Mtego anamtega na kumwingiza Mwakuona kwenye danguro. Mwakuona anajiandaa kwenda ng’ambo kama ahadi ilivyosema, lakini anapotolewa kwenye maandalizi, anaelekezwa Chenga-ways ambako biashara ya ufuska inaendeshwa.
Mwakuona anapofika, mwanamapokezi anamwambia kuwa kuna watatu wanaomng’ang’ania. Mwakuona anafikiri anarejelea waajiri. Anasikia vicheko nyuma ya kaunta. Hali halisi ni kwamba ni wanaume wanaomng’ang’ania ili wazini naye kwa kuwa ni mrembo sana.
Mwakuona anawaona wanawake ambao wamevaa nusu uchi wakitembea kwa madaha mbele ya wanaume huku wakiwakagua. Wanaume wanachagua wanaotaka, ambao wanaelekezwa katika chumba fulani. Wanaume hawa wanalipa na kuelekea kutimiza ashiki zao. Anapoelekezwa kwenye chumba chake, anaona wanaume wamekalia viti kama huko alikotoka, wanachagua wasichana kati ya wanaonengua viuno mbele yao, huku wamevaa viguo vinavyoning’inia viunoni. Mwakuona anapoelekezwa chumbani mwake, kuna wanume
wanaokutana nao, ambao wanageuka tena kumwangalia. Anakutana na msichana waliyekuwa pamoja maandalizini. Anataka kumpiga pambaja lakini mwanamapokezi anamzuia. Msichana yule anamwambia kuwa atajulia huko mbele. Yeye ashayajua tayari.
Mwakuona hatimaye anafikishwa kwenye chumba, kuongozwa ndani na mlango kukomelewa. Anamkuta mwanamume ambaye anamsifia kwa urembo wake na kumweleza kwamba ameshalipa kwa ajili yake. Mwakuona anajaribu kubisha akisema yeye si kahaba, lakini tayari ashafika kichijioni, hana namna ya kujiopoa.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 11:45


Next: Je, anwani Pupa inafaa? Fafanua.
Previous: Eleza mbinu zifuatazo zilivyotumika kwenye hadithi, Pupa, ukitolea mifano; i. Kinaya ii. Sadfa

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions