Eleza mbinu zifuatazo zilivyotumika kwenye hadithi, Pupa, ukitolea mifano; i. Kinaya ii. Sadfa

      

Eleza mbinu zifuatazo zilivyotumika kwenye hadithi, Pupa, ukitolea mifano;
i. Kinaya
ii. Sadfa

  

Answers


Francis
i. Kinaya
Wakazi wa Mwinamo, licha ya kuwa wanazugwa na umaskini, wanakopoa watoto wengi. Wanaona kuwa wanaweza kupata wa kuwafaa kati yao. La ajabu ni kuwa hawawazii jinsi watakavyowalisha watoto hao kwa hali hiyo.
Rai ya Bi. Mtego kuwa Mwakuona asiwajuze wazazi wake haimpigi mshipa. Ni kinaya kwake kushikilia kuwa wazazi hawafai kujua hadi mipango inapotamatika. Kwa nini wasijue hali ni mwanao? Ni wazi kwamba huu ni unafiki lakini Mwakuona hatambui hilo.
Ni kinaya kuwa Mwakuona haoni dalili zote kuwa Bi. Mtego anamhadaa. Anayemsaidia bado ndiye anamhudumia, jambo ambalo halimpigi mshipa. Hata wanapofika kwenye danguro, bado akili yake inamwambia kuwa anaenda ng’ambo wala yanyotukia pale hayamhusu.
Mwakuona anamwuliza mhudumu kwenye kaunta kuhusu safari yake ya ng’ambo. Anashangaa kwa nini hawakuamua kuhusu mwajiri wake anapoambiwa kuna watu watatu wanaomng’ang’ania. Ni wazi kwamba haya ni masuala tofauti na kazi ya ng’ambo. Hawazii haya angaa kujaribu kujinasua.
Ni kinaya kuwa kati ya wasichana wengi waliokuwa matayarishoni, hakuna hata mmoja aliyewaza kuhusu waliyokuwa wakiandaliwa, licha ya dalili kuwa wazi.
Mwakuona anaondoka nyumbani kwa matumaini makuu ya kuiboresha hali yake na ile ya aila yake. Ajabu ni kuwa badala yake, anarejea akiwa maskini zaidi, wa mali na utu!

ii. Sadfa
Mwakuona anakutana na Bi. Mtego kisadfa akitoka shuleni bila kumtarajia.
Mwakuona anapomfuata mwelekezi kuelekea asikokujua, anakutana kisadfa na msichana waliyekuwa pamoja kwenye ‘matayarisho’ japo hawapatiwi fursa ya kuwasiliana.
Mashaka na Mwakuona wanakutana kisadfa, baada yake kuhujumiwa kule danguroni. Wanaishia kuwa na kisa kinacholingana na kuwa marafiki wa kutiana moyo.
Mwakuona anafaulu kutoroka kisadfa. Anaenda msalani usiku wa manane bila kuandamwa, kinyume na taratibu. Isitoshe, inasadifu kuwa choo hicho kiko pembeni na kina bati lililobambatuka, linalompa mwanya wa kuhepea.
Wakati wa kutoroka, anamsikia mtu upande wa pili akikemea kisha vishindo vyake akitoroka. Hakutarajia kumpata yeyote pale wakati huo.
Mwakuona anatoroka usiku wa manane na kujaribu kutafuta njia ya kurudi kwao Mwinamo asiijue. Kunapopambazuka na jua kuchomoza, anakuona Mwinamo kwa mbali.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 11:48


Next: Umaskini na usherati ni baadhi ya mambo ambayo hudidimisha maendeleo. Thibitisha kauli hii ilivyotumika katika hadithi, Pupa.
Previous: Utanzu wa ushairi umepitia matapo/vipindi vinne katika kukua na kusambaa kwake. Eleza vipindi kama vinavyoelezewa na Kitula King’ei na Amata Kemoli, katika Diwani yao ‘Taaluma...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions