Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Wanafunzi wengi hushindwa kueleza maana ya ushairi. Dhana ya ushairi inaweza kufafanuliwa kwa njia kadhaa.
Ushairi ni mojawapo wa utanzu wa fasihi andishi unaoelezea mawazo mazito kuihusu jamii na ulio na mpangilio mahsusi wa maneno yenye mtiririko, lugha ya mkato na urembo fulani wa aina yake.
Ni sanaa inayotambulishwa na mpangilio maalum wa vifungu ambao una mdundo maalum na aghalabu hutumia lugha ya mkato.
Shairi ni utungo wa kisanaa ambao hutumia lugha teule na kushirikisha mpangilio maalum wa maneno ili kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa. Ni tungo za kishairi zenye maudhui maalum yanayomhusu mwanadamu na tabia zake.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 12:31