Eleza aina tofauti za mishororo katika ubeti

      

Eleza aina tofauti za mishororo katika ubeti

  

Answers


Francis
i. Mwanzo –ni mshororo wa kwanza katika ubeti. Pia huitwa fatahi ama kifungua.
ii. Mloto – ni mshororo wa pili katika ubeti.
iii. Mleo – ni mshororo wa tatu katika ubeti.
iv. Mshata (mishata)- ni mshororo katika ubeti wa shairi ambao haujakamilika haswa kimaana na hutegemea mwingine unaofuata ili kupasha ujumbe. Idadi ya mizani pia huweza kuwa si kamilifu ikilinganishwa na mishororo mingine.
v. Mistari kifu/toshelezi- ni mishororo inayojitosheleza kimaana bila kutegemea mishororo mingine. Vilevile idadi ya mizani huwa kamili katika mishororo yote.
vi. Kibwagizo/kiitikio/mkarara/kipokeo – Aghalabu huwa ni mshororo wa mwisho katika ubeti ambao umerudiwarudiwa katika beti zote.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 13:06


Next: Ni nini maana ya mshororo mishororo
Previous: Eleza maana na umuhimu wa kibwagizo.

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions