Eleza maana ya arudhi

      

Eleza maana ya arudhi

  

Answers


Francis
Hizi ni sheria au kanuni zinazotawala utunzi wa mashairi. Suala hili la arudhi haswa hujitokeza sana katika mashairi ya jadi. Kanuni hizi ni kama vile: urari wa vina, mpangilio maalum wa beti, mishororo sawa katika kila ubeti, mizani inayojitosheleza katika kila mshororo, vipande sawa katika kila mshororo n.k.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 13:38


Next: Eleza maana ya utoshelezo katika ushairi
Previous: Eleza maana ya muwala

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions