Fafanua migao/kategoria mbili kuu za mashairi

      

Fafanua migao/kategoria mbili kuu za mashairi

  

Answers


Francis
1. Mashairi ya jadi.
Mashairi haya pia huitwa mashairi ya kimapokeo au ya kiarudhi. Aina hii ya mashairi hufuata kaida za utunzi wa mashairi. Kanuni hizi ni kama vile:
- urari wa vina
- mpangilio maalum wa beti
- mishororo sawa katika kila ubeti
- mizani inayojitosheleza katika kila mshororo
- vipande sawa katika kila mshororo n.k.
Malenga wanaoshikilia msimamo huu huitwa wanamapokeo. Mashairi yasiyofuata sheria hizi hujulikana kama guni.

2. Mashairi huru/za kisasa
Ni kategoria ya mashairi yasiyozingatia kanuni za utunzi. Hii ina maana ya kwamba kanuni zilizoorodheshwa chini ya mashairi ya kimapokeo siyo lazima zifuatwe. Aghalabu mashairi haya huzingatia maudhui kwa kina. Kila malenga huwa na mtindo wake tofauti wa kuwasilisha kazi yake. Wanaoshikilia msimamo huu nao huitwa wanamapinduzi. Mashairi haya pia huitwa mapingiti/mavue/ masivina/zuhali/za kimapinduzi.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 13:54


Next: Eleza maana za istilahi zifuatazo za ushairi; i. Bahari ii. Diwani
Previous: Nimeyaandika maneno haya kwa niaba ya, Mamilioni wasio malazi Wazungukao barabarani bila mavazi Wabebao vifurushi vilivyo wazi, … milki yao ya maisha. Kwa niaba ya: Maelfu wanaovuma bila haki Wiki baada ya wiki Leo...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions