Nimeyaandika maneno haya kwa niaba ya, Mamilioni wasio malazi Wazungukao barabarani bila mavazi Wabebao vifurushi vilivyo wazi, … milki yao ya maisha. Kwa niaba ya: Maelfu wanaovuma bila haki Wiki baada ya wiki Leo...

      

Nimeyaandika maneno haya
kwa niaba ya,
Mamilioni wasio malazi
Wazungukao barabarani bila mavazi
Wabebao vifurushi vilivyo wazi,
… milki yao ya maisha.

Kwa niaba ya:
Maelfu wanaovuma bila haki
Wiki baada ya wiki
Leo sumu au spaki
Leo kamba au bunduki
Na kwa wale wanasubiri kunyongwa

Kwa niaba ya
Vijana walio mtaani
Wale mayatima na maskini
Wazungukao mapipani
Kila pembe mjini
Kuokota sumu kutia tumboni
Kujua bila kujua
’ili kupata kuishi.

Kwa niaba ya:
Wakongwe wasiojiweza
Walao chakula kilichooza
Wachukuao choo wakijipakaza
Pole pole wakijiangamiza
Katika vyumba vyao
Baridi na giza
Kwa saba hawan watazama
Wala wauguza


Eleza sababu za kuliita shairi hili huru

  

Answers


Francis
- Halina urari wa vina
- Mizani si sawa katika mishororo yake
- Idadi ya mishororo katika beti ni tofauti
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 13:57


Next: Fafanua migao/kategoria mbili kuu za mashairi
Previous: Taja sifa za mashairi huru

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions