Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini Naja kwingine kuwapi,...

      

Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo
Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando
Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo
Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini

Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo?
Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?
Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

Naja nije rudi papo, panigedeme mgando
Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo
Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
(Limenukuliwa)


Tunaainisha shairi hili kama la jadi kwa sababu:

  

Answers


Francis
- Lina urari wa vina
- Lina mishororo sawa (minne) katika kila ubeti
- Mizani inajitosheleza katika kila mshororo (mizani 16)
- Vipande ni sawa (viwili, yaani ukwapi na utao) katika kila mshororo
- Lina beti tatu zinazojitosheleza.
francis1897 answered the question on January 30, 2023 at 14:04


Next: Taja sifa za mashairi huru
Previous: Taja visawe vya mashairi ya jadi

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions