Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti

      

Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti

  

Answers


Francis
1. Tathmina/umoja – ni shairi lenye mshororo mmoja katika kila ubeti. Mashairi ya aina hii hayapatikani kwa wingi.

2. Tathnia/uwili – ni shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti. Mashairi haya ingawaje yapo, lakini pia kwa uchache.

3. Tathlitha/utatu/wimbo – ni shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti. Shairi la aina hii wakati mwingine pia huitwa wimbo.

4. Tarbia/unne – ni shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti. Mashairi mengi ambayo yametungwa huwa ni ya aina hii.

5. Takhmisa/utano – ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti.

6. Tasdisa/usita – ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti.

7. Tasbia/usaba – ni shairi lenye mishororo saba katika kila ubeti.

8. Naudi/unane – ni shairi lenye mishororo minane katika kila ubeti.

9. Telemania/utisa – ni shairi lenye mishororo tisa katika kila ubeti.

10. Ukumi – ni shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti. Pia shairi hili huitwa ushuri.

11. Soneti- ni shairi lenye mishororo kumi na minne katika kila ubeti.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 06:23


Next: Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.
Previous: Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions