Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo

      

Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo

  

Answers


Francis
a) Utenzi
Ni bahari ambapo shairi huwa na kipande kimoja katika kila mshororo. Mengi ya mashairi haya huwa ni marefu sana. Mashairi haya aghalabu huwa na mizani zisizozidi 12 katika mshororo na huzungumzia maswala mazito kama vile siasa, dini na ndoa. Mfano wa utenzi ni kama vile Utenzi wa Mwana Kupona.

b) Mathnawi
Ni bahari ambapo shairi huwa na vipande viwili katika kila mshororo yaani ukwapi na utao.

c) Ukawafi
Ni bahari ambapo shairi huwa na vipande vitatu katika kila mshororo yaani ukwapi, utao na mwandamizi.

d) Bantudi/Tuo
Ni bahari ambapo shairi lina vipande vinne katika kila mshororo yaani ukwapi, utao, mwandamizi na ukingo.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 06:31


Next: Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti
Previous: Eleza aina za mashairi kulingana na vina

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions