Eleza aina za mashairi kulingana na vina

      

Eleza aina za mashairi kulingana na vina

  

Answers


Francis
a) Mtiririko
Katika bahari hii, shairi huwa na vina vya kati/ndani na vilevile vina vya nje ambavyo havibadiliki katika utungo mzima. Hii ina maana kuwa vina vya ndani vinafululiza katika beti zote na vilevile vina vya nje pia vinafululiza katika beti zote.

b) Ukara
Bahari hii ya shairi huwa na vina vya kipande kimoja ambavyo havibadiliki katika utungo mzima, lakini vina vya kipande kingine vinabadilika kutoka ubeti hadi mwingine.

c) Ukaraguni
Ni bahari ya shairi ambalo vina vyake vya ukwapi, utao, mwandamizi au ukingo huwa vinabadilika baina ya beti, yaani vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Hii ina maana ya kuwa vina vya ndani na vya nje huwa ni tofauti katika beti zote.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 06:37


Next: Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo
Previous: Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions