Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo: a) Sakarani b) Ngonjera c) Malumbano d) Masivina e) Taabili f) Mandhuma g) Kisarambe h) Mavue i) Sabilia j) Togoo k) Kumbukizi

      

Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
a) Sakarani
b) Ngonjera
c) Malumbano
d) Masivina
e) Taabili
f) Mandhuma
g) Kisarambe
h) Mavue
i) Sabilia
j) Togoo
k) Kumbukizi

  

Answers


Francis
a) Sakarani
Huwa ni mchanganyiko wa bahari mbalimbali katika shairi moja. Kwenye ubeti mmoja, kunakuwa na bahari tofauti, kwa mfano ubeti wa kwanza ni wa aina ya tathlitha, ubeti wa pili ni wa takhmisa n.k.

b) Ngonjera
Ni shairi la majibizano. Tofauti na tungo nyinginezo, ngonjera hukaririrwa, haziimbwi. Ngonjera hutambuliwa kwa kuwepo kwa wahusika wanaojibizana katika utungo. Pia huambatana na vitendo.

c) Malumbano
Ni shairi lenye mjadala juu ya jambo fulani, yakiwa ya kupinga, kuunga mkono,
kuonya au kusifu. Huwa ni mashairi ya mafumbo, kwa hivyo kwa njia ya kishairi,
malenga kadhaa hufumbiana ama kujibizana. Aghalabu huwa ni mashairi mawili.

d) Masivina
Ni bahari la shairi lisilo na urari wa vina katika mishororo yake. Hii ina maana
kuwa vina vyake vyote aidha vya kati au vya nje vinatofautiana baina ya mishororo.

e) Taabili
Ni shairi ambalo limetungwa kwa nia ya kumsifu mtu aliyeaga dunia.

f) Mandhuma
Ni bahari ya shairi ambalo upande mmoja (ukwapi) hueleza hoja au huuliza
swali na kisha upande wa pili (utao) hutoa jibu au suluhu ya swali hilo.

g) Kisarambe
Ni shairi ambalo haswa limejikita kwa maudhui ya kidini. Huweza kuitwa pia kasida.

h) Mavue
Ni aina ya mashairi yasiyofungika na sheria zozote za kiarudhi kama vile utoshelezi wa vina na mizani.

i) Sabilia
Ni shairi ambalo halina kibwagizo bali huwa na mstari wa kituo/ kiishio/ kimalizio.

j) Togoo
Ni aina ya shairi ambalo limetungwa kwa kusudi la kusifia uzuri wa mahali, mtu au kitu fulani.

k) Kumbukizi
Ni aina ya shairi ambalo huwakumbusha watu kuhusu matukio mahsusi katika jamii. Matukio haya yaweza kuwa ya kihistoria, kidini au hata kishujaa. Kwa mfano ujio wa Rais wa Marekani nchini Kenya, ujio wa Papa Mtakatifu (2015) ni matukio ya kihistoria.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 07:09


Next: Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani
Previous: Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions