Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi

      

Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi

  

Answers


Francis
a) Dhamira
Mara si haba, wanafunzi hukumbana na swali hili…‘Eleza dhamira ya shairi hili.’ Dhamira ni lengo kuu ambalo malenga huwa nalo anapoitunga kazi yake. Lengo la mtunzi linaweza kuwa kuelimisha jamii, kuikosoa jamii, kutahadharisha, kufariji, kuhamasisha n.k Maneno mengine ambayo huweza kutumika badala ya dhamira ni kama vile lengo, nia, kusudi, azma.

b) Maudhui
Suala la maudhui ni muhimu sana katika uchambuzi wa mashairi na hata kazi nyinginezo zozote za fasihi. Maudhui ni ujumbe mkuu unaowasilishwa katika kazi ya fasihi. Maudhui huweza kuwa kama vile ya ndoa, migogoro, elimu, matabaka, ukengeushi n.k

c) Muundo
Ni kawaida vilevile wanafunzi kuulizwa…‘Eleza muundo wa hili shairi.’ Muundo ni mjengo, umbo au sura ya shairi. Umbo hubainishwa kwa kuonekana bayana kama alivyoandika mtunzi. Mwanafunzi anapolijibu swali hili anastahili kuangalia shairi na kuandika tu anayoyaona. Hastahili kufikiria kwa kina ili kuandika anayoyaona.

d) Lugha
Matumizi ya lugha na viambajengo vyake ni muhimu sana katika kufanikisha uchambuzi bora wa mashairi. Jinsi malenga mmoja anavyotumia lugha ni tofauti sana na jinsi malenga mwingine atakavyoitumia. Kipengele hiki huchunguza jinsi mtunzi ametumia tamathali za usemi. Lugha pia huendeleza maudhui ya shairi.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 07:12


Next: Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo: a) Sakarani b) Ngonjera c) Malumbano d) Masivina e) Taabili f) Mandhuma g) Kisarambe h) Mavue i) Sabilia j) Togoo k) Kumbukizi
Previous: Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions