Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi

      

Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi

  

Answers


Francis
? Tashbihi/mshabaha- ni mbinu ya lugha ambapo vitu viwili hulinganishwa kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Kwa ufupi,ni ulinganisho isiyo wa moja kwa moja kwa kutumia vilinganishi kwa mfano: mithili ya, kama, ja na sawa na. Tazama mfano huu: Juma ni mrefu mithili ya/ja mlingoti.

? Uhaishaji/uhuishi/tashihisi- ni mbinu ambayo vitu visivyo na uhai hupewa sifa za kibinadamu. Mfano: Kaburi likammeza mzima mzima.

? Misemo na nahau- ni kauli fupifupi ambazo hutumika kutoa maana nyingine pasi na maana iliyotumika. Misemo huwa haitumii vitenzi kwa mfano: mkono birika- mchoyo, mkono mrefu-mwizi n.k. Nahau hutambulishwa kwa matumizi ya vitenzi kwa mfano: kula kalendafungwa jela, chungulia kaburi- karibia kifo n.k

? Takriri/anafora- mbinu ya kurudiarudia neno,tukio au mawazo Fulani.

? Maswali balagha/mubalagha- huwa ni maswali yasiyohitaji majibu.

? Tanakuzi- pia huitwa ukinzani. Hapa mawazo yanayokinzana hutumiwa pamoja katika sentensi moja. Kwa mfano; baada ya dhiki faraja, mpanda ngazi hushuka, nazama nakuibuka.

? Tanakali za sauti- mbinu hii pia hujulikana kama onomatopeia. Maneno yanayoiga sauti au hali fulani hutumika. Mfano kuanguka majini chubwi.

? Methali- huwa ni misemo ya hekima na ambayo maana yake imefumbwa. Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Mbinu iliyotumika katika uundaji wa istilahi hizo za majina ni ile ya kuunganisha viambishi awali vya maneno yanayopatikana katika kila kikundi.

? Chuku/udamizi- ni mbinu ya kutilia chumvi suala fulani kwa ajili ya kusisitiza ujumbe fulani.

? Tasfida- ni matumizi ya lugha ya adabu ili kuficha makali ya lugha. Mfano kujifungua mtoto badala ya kuzaa, kuenda haja badala ya kuenda chooni.

? Kinaya- hapa mtunzi huleta dhana ya kinyume cha matarajio. Kwa mfano badala ya kiongozi alichaguliwa kutetea maslahi ya watu wake akawa wa kwanza kuwanyanyasa. Kuna aina kadhaa za kinaya kama vile kinaya cha kiusemi na kinaya hali. Kinaya cha kiusemi ni hali ambapo maana inayokusudiwa huwa kinyume cha kile kinachosemwa. Katika kinaya hali matokeo huwa kinyume cha matarajio.

? Jazanda- matumizi ya lugha fiche au ya mafumbo. Msomaji huhitajika kuwaza maana kamili iliyokusudiwa. Kwa mfano paka na panya kwa maana ya watawala na watawaliwa, Mdudu hatari kurejelea ugonjwa wa UKIMWI.

? Tabaini- matumizi ya neno “si” pamoja na maneno kinzani. Kwa mfano: Alikuwa si wa maji si wa dawa.

? Utohozi- mbinu ya kuswahilisha maneno yasiyo ya lugha ya Kiswahili. Mfano “school”- skuli, “Class”- klasi

? Sitiara/sitiari- huu ni ulinganisho wa vitu au hali mbili kwa njia ya moja kwa moja kwa sababu vitu hivi vina sifa au tabia sawa. Mfano: Mwalimu mkuu ni simba, Maria ni twiga.

? Taashira/Ishara - mbinu ambapo mtunzi hutumia lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Kwa mfano mvi kuashiria mtu mzee.

? Taswira- ni mbinu ambapo mtunzi hutoa maelezo ambayo huibua picha ya kitu au hali fulani akilini mwa msomaji.

? Nidaa/siahi- hutambulishwa na matumizi ya alama hisi (!) ambayo mtunzi hutumia kudhihirisha hisia fulani kama vile furaha, huzuni, mshangao n.k

? Majazi- mbinu ya mwandishi kuwapa wahusika ama mahali majina yanayoshabihiana na tabia, vitendo au hali zao.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 07:27


Next: Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi
Previous: Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions