Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi

      

Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi

  

Answers


Francis
1) Mazida – uhuru huu humruhusu mtunzi kuyarefusha maneno fulani. Mazida husaidia kuleta utoshelezo wa idadi ya mizani katika kipande au mshororo na pia urari wa vina.
2) Inkisari – huu ni uhuru wa mshairi kuyafupisha maneno fulani. Kama ilivyo katika mazida, inkisari pia husaidia kutosheleza idadi ya mizani na kuleta urari wa vina.
3) Tabdila – ni uhuru wa mshairi kubadilisha herufi au hata sauti ya neno bila kubadili maana ya neno hilo. Kwa mfano daraza badala ya darasa. Tabdila husaidia kuleta urari wa vina katika kipande cha mshororo.
4) Kuboronga/kufinyanga/Kubananga sarufi – pia huitwa miundo ngeu/ukiushi wa kisintaksia/ukiushi wa kimiundo. Huu ni uhuru wa mshairi kutofuata kanuni zinazotawala sarufi. Kusudi la kufanya hivi ni kuleta urari wa vina katika mishororo. Kwa mfano, kunapopambazuka kila, amka mwanadamu badala ya kila kunapopambazuka, mwanadamu amka
5) Kikale – ni matumizi ya msamiati wa kale, kwa mfano, nyuni badala ya ndege, mgunda badala ya shamba n.k
6) Vilugha/vilahaja – ni matumizi ya msamiati wa lahaja za Kiswahili badala ya Kiswahili sanifu.
7) Utohozi – kutohoa ni kuswahilisha msamiati wa lugha nyingine na kuwa Kiswahili. Kwa mfano, klasi badala ya class, eropleni badala ya aeroplane, deski badala ya desk n.k.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 08:43


Next: Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi
Previous: Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana,...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions