Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana,...(Solved)
Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
(Abdalla Said Kizere)
Maswali
a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
d) Eleza umbo la shairi hili.
e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi (Solved)
Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi(Solved)
Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi(Solved)
Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema...(Solved)
Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Taja majina yanayopendekezwa
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi(Solved)
Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi(Solved)
Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi(Solved)
Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi(Solved)
Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
a) Sakarani
b) Ngonjera
c) Malumbano
d) Masivina
e) Taabili
f) Mandhuma
g) Kisarambe
h) Mavue
i) Sabilia
j) Togoo
k) Kumbukizi(Solved)
Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
a) Sakarani
b) Ngonjera
c) Malumbano
d) Masivina
e) Taabili
f) Mandhuma
g) Kisarambe
h) Mavue
i) Sabilia
j) Togoo
k) Kumbukizi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani(Solved)
Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno(Solved)
Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Eleza aina za mashairi kulingana na vina(Solved)
Eleza aina za mashairi kulingana na vina
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo(Solved)
Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti (Solved)
Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.(Solved)
Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Nini maana ya bahari za mashairi?(Solved)
Nini maana ya bahari za mashairi?
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
Taja visawe vya mashairi huru(Solved)
Taja visawe vya mashairi huru
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
Taja visawe vya mashairi ya jadi(Solved)
Taja visawe vya mashairi ya jadi
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo
Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando
Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo
Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini
Naja kwingine kuwapi,...(Solved)
Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo
Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando
Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo
Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini
Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo?
Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?
Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
Naja nije rudi papo, panigedeme mgando
Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo
Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando
Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini
(Limenukuliwa)
Tunaainisha shairi hili kama la jadi kwa sababu:
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)