Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona...

      

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili

Lakini

Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi

Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
Ile sauti zamani kidogo
“Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima nifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka

Jambo moja nakukumbukia: Mungu
Je, nimwombe tena? Hadi lini?
Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!

Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.


(a) Eleza toni ya shairi hili.
(b) Tambua nafsineni katika shairi hili.
(c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti wa tatu?
(d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka.
(e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
(f) Eleza maana ya:
(i) kuruba
(ii) barabara yenye ukungu

  

Answers


Francis
(a) Toni ya kuhimiza/matumaini/matarajio
(b) Msafiri/mwenye matumaini katika maisha
(c) Kuwa tayari kupambana na misukosuko utakayokutana nayo
(d)
- Taswira- miinuko
- Tasihisi- azma kunihimiza
- Tanakuzi- zama na kuibuka
- Taashira- barabara- maisha, miinuko- ugumu
- Jazanda/stiari- barabara
(e) Nafsineni ni Mcha Mungu- dini
(f)
- kuruba- mahangaiko/mateso
- barabara yenye ukungu- misukosuko
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 09:19


Next: Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami...
Previous: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Daima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions