Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Daima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa...

      

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.

Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi za maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
kumpapasa,kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha …

Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani
katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama si kujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laiti angalijua!
(T. Arege)

Maswali
a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.
c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili.
d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:
i. tashhisi
ii. kinaya
iii. tashbihi
f) Eleza toni ya shairi hili.
g) Bainisha nafsineni katika shairi hili.
h) Changanua muundo wa shairi hili.

  

Answers


Francis
a)
? Mwenye tumaini/tama- kubwa hamu
? Mwenye bidii- alfajiri na mapema, kutokwa na jasho
? Anayeyafurahia mandhari- anapotembea anasikiliza videge…
? Mtulivu- kuna siri gani inayomliwaza?
? Aliyedhulimiwa- soko la dunia lamkaba koo.
? Anayesagika kwa kazi ngumu kuwafaida wenye tama- ayalimia matumbo ya waroho.
? Aliyeridhika- kuna jambo gani linalomridhisha.

b)
? Inkisari- babuze- babu zake
? Kufinyanga sarufi/miundo ngeu ya kisintaksia- kubwa hamu- hamu kubwa

c)
? Taswira mnuso/harufu- rihi ya maua
? Taswira mguso- kumpapasa, kumbusu miguu
? Taswira usikivu- anasikiliza ndege
? Taswira ya mwendo- yeye kuendelea kwa furaha

d)
Maswali ya balagha yametumiwa:
? Kudadisi hali/kushangaa- kuna siri gani inayomliwaza? Kuna jambo gani linalomridhisha?
? Kuonyesha hali ya kinyume, kutokubaliana na jambo- furaha ya mtu ni furaha gani, katika dunia inayomhini?
? Kuzindua- furaha ya mtu ni furaha gani, katika dunia inayomhini?

e)
? Tashhisi- umande kumbusu, miti kumpapasa
? Kinaya- mkulima anafurahi ilhali dunia inamhini
? Tashbihi- kama mtu aliye na kubwa hamu

f)
? Toni ya uchungu- furaha ya mtu ni furaha gani katika jamii inayomhini?
? Toni ya kuajabia/kushangazwa na jambao- kuna jambo gani linalomridhisha?
? Kuhuzunisha/kusikitisha/kuhurumia

g) Nafsineni ni:
? Mtetezi wa haki/mtu aliyezinduka/anayelalamikia dhuluma ya wanyonge
? Mtu anayemtazama mkulima akipita

h)
? Shairi lina beti tatu
? Kila ubeti una idadi tofauti ya mishororo na beti nyingine
? Kila mshororo una kipande kimoja
? Shairi halina mpangilio maalum wa vina
? Idadi ya mizani katika mishororo inatofautiana
? Mshororo wa mwisho katika kila ubeti ni tofauti/ kituo/kimalizio/ kiishio
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 09:24


Next: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona...
Previous: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Mwili Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili. Vitisho kamwe...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions