Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Mwili Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili. Vitisho kamwe...

      

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili

Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.

Vitisho kamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.

Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.

Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.

Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.


a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
c) Eleza toni ya shairi hili.
d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili?
e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande.
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.

  

Answers


Francis
a)
? Dhamira ya mwandishi ni kuonyesha kuwa kazi ni shughuli muhimu ila haiwezi kuzingatiwa zaidi ya afya.
? Kuonyesha kuwa ipo haja ya kuipa afya kipaumbele kwa kuvikataa vitisho vya wenye kazi/waajiri.
? Kuonyesha dhuluma wanazofanyiwa wafanyakazi vitisho pamwe kelele.
? Kuukosoa uongozi dhalimu- kufutwa sikawi
? Kuzindua wafanyakazi

b)
? Shairi linatumia Kiswahili sanifu
? Kuna matumizi ya sitiari/jazanda- si gurudumu mwili
? Uhaishaji- ugonjwa umepewa sifa ya kutenda mwili kuudhili
? Matumizi ya nahau- viraka kuutia (ub 3)
? Urudiaji wa maneno/takriri- kila ubeti unaisha kwa neno mwili

c) Toni ya:
? Hasira- si gurudumu mwili
? Ukali- sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili. Kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili
? Machungu- ila wauma mwili
? Kukashifu- vitisho pamwe kelele, ninavicha
? Kulalamika- sihofu kupata mawi, sitajuta

d) Mwenye kazi/mwajiri

e) Ukawafi-vipande vitatu katika kila mshororo.

f) Mimi kwa hakika ninaithamini kazi kwa akili na mwili/isipokuwa siamini kwamba inafaa kuteseka kwa kila hali. Hasa ugonjwa unapohusika kutumia nguvu hakuwezi kunitisha/siwezi kuogopa kutumia nguvu kujitetea.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 09:33


Next: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Daima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa...
Previous: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza 1 Ngakua na mato, ya kuonea Ngalisana kito,cha kuchezea Kilicho kizito, cha kuelea Kikamuenea,...

View More Ushairi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Daima alfajiri na mapema Hunipitia na jembe na kotama Katika njia iendayo kondeni Kama walivyofanya babuze zamani; Nimuonapo huwa anatabasamu Kama mtu aliye na kubwa...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    Daima alfajiri na mapema
    Hunipitia na jembe na kotama
    Katika njia iendayo kondeni
    Kama walivyofanya babuze zamani;
    Nimuonapo huwa anatabasamu
    Kama mtu aliye na kubwa hamu
    Kushika mpini na kutokwa jasho
    Ili kujikimu kupata malisho.

    Anapotembea anasikiliza
    Videge vya anga vinavyotumbuiza
    Utadhani huwa vimemngojea
    Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
    Pia pepo baridi kumpepea
    Rihi za maua zikimletea
    Nao umande kumbusu miguu;
    Na miti yote hujipinda migongo
    kumpapasa,kumtoa matongo;
    Na yeye kuendelea kwa furaha
    kuliko yeyote ninayemjua
    Akichekelea ha ha ha ha ha ha …

    Na mimi kubaki kujiuliza
    Kuna siri gani inayomliwaza?
    Au ni kujua au kutojua?
    Furaha ya mtu ni furaha gani
    katika dunia inayomhini?
    Ukali wa jua wamnyima zao
    Soko la dunia lamkaba koo;
    Dini za kudhani zamsonga roho
    Ayalimia matumbo ya waroho;
    Kuna jambo gani linamridhisha?
    Kama si kujua ni kutokujua
    Laiti angalijua, laiti angalijua!
    (T. Arege)

    Maswali
    a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
    b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.
    c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili.
    d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
    e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:
    i. tashhisi
    ii. kinaya
    iii. tashbihi
    f) Eleza toni ya shairi hili.
    g) Bainisha nafsineni katika shairi hili.
    h) Changanua muundo wa shairi hili.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
    T. Arege: Barabara
    Barabara bado ni ndefu
    Nami tayari nimechoka tiki
    Natamani kuketi
    Ninyooshe misuli
    Nituliza akili

    Lakini

    Azma yanisukuma
    Mbele ikinihimiza kuendelea
    Baada ya miinuko na kuruba
    Sasa naona unyoofu wake
    Unyoofu ambao unatisha zaidi

    Punde natumbukia katika shimo
    Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
    Ghafla nakumbuka ilivyosema
    Ile sauti zamani kidogo
    “Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

    Ingawa nimechoka
    Jambo moja li dhahiri
    Lazima nifuate barabara
    Ingawa machweo yaingia
    Nizame na kuibuka
    Nipande na kushuka

    Jambo moja nakukumbukia: Mungu
    Je, nimwombe tena? Hadi lini?
    Labda amechoshwa na ombaomba zangu
    Nashangaa tena!

    Kitu kimoja nakiamini
    Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
    Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
    Nikinaswa na kujinasua
    Yumkini nitafika mwisho wake
    Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.


    (a) Eleza toni ya shairi hili.
    (b) Tambua nafsineni katika shairi hili.
    (c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti wa tatu?
    (d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka.
    (e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
    (f) Eleza maana ya:
    (i) kuruba
    (ii) barabara yenye ukungu

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami...(Solved)

    Kilio cha Lugha
    Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
    Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
    Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
    Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia

    Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
    Hamna nami imani, wala kupanga siasa
    Mwasema sayansini, siku ningalitosa
    Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika

    Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu
    Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu
    Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu
    Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.

    Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza
    Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
    Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza
    Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

    Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza
    Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza
    Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza
    Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

    Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao
    Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
    Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
    Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

    Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia
    Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
    Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria
    Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia

    Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote
    Msamiati huwa, ni wa Afrika yote
    Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote
    Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

    Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi
    Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi
    Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
    Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha

    Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya
    Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya
    Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya
    Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

    Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana
    Kukua imeridhia, msamiati kufana
    Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana
    Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia.


    Maswali
    (a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu
    (b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha.
    (c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
    (d) Eleza toni ya shairi hili.
    (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu.
    (f) Bainisha nafsineni katika shairi.
    (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
    i. nasongwa
    ii. kuriaria
    iii. adinasi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Lau dunia nanena, tuseme si ati ati, Mauti kawa hakuna, katika wote wakati, Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati? Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana? Dunia ingetatana, na kizazi katikati, Huku kwazaliwa bwana,...(Solved)

    Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
    Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
    Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
    Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
    Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
    Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
    Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?

    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
    Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
    Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
    Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
    Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
    Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
    Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
    Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Peleleza utaona, hayataki utafiti,
    Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
    Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

    Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
    Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
    Yote tuloelezana, katenda bila senti,
    Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
    (Abdalla Said Kizere)


    Maswali
    a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
    b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
    c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
    d) Eleza umbo la shairi hili.
    e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
    f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
    g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi (Solved)

    Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi(Solved)

    Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi(Solved)

    Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema...(Solved)

    Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Taja majina yanayopendekezwa

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi(Solved)

    Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi(Solved)

    Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi(Solved)

    Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi(Solved)

    Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo: a) Sakarani b) Ngonjera c) Malumbano d) Masivina e) Taabili f) Mandhuma g) Kisarambe h) Mavue i) Sabilia j) Togoo k) Kumbukizi(Solved)

    Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
    a) Sakarani
    b) Ngonjera
    c) Malumbano
    d) Masivina
    e) Taabili
    f) Mandhuma
    g) Kisarambe
    h) Mavue
    i) Sabilia
    j) Togoo
    k) Kumbukizi

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani(Solved)

    Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno(Solved)

    Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Eleza aina za mashairi kulingana na vina(Solved)

    Eleza aina za mashairi kulingana na vina

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo(Solved)

    Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti (Solved)

    Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.(Solved)

    Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)

  • Nini maana ya bahari za mashairi?(Solved)

    Nini maana ya bahari za mashairi?

    Date posted: February 1, 2023.  Answers (1)