a)
? Shairi linazungumzia tatizo la upofu mf. ngakua na mato.
? Kwamba mtu anayepatwa na tatizo la upofu huwa hawezi kufanya mambo ambayo zamani alizimudu bila tatizo.
? Nafsineni inasikitikia hali yake ya kutomudu kujifanyia mambo kwa sababu ya upofu.
b)
? Inkisari- imetumika ili kudumisha ulinganifu wa mizani. Mf. ngaliandaa- ningaliandaa, ngalifanya- ningalifanya, ngatia- ningalitia
? Tabdila- imetumiwa ili kuleta urari wa vina mf. mduwaa- mduara, apikae- apikaye
? Kuboronga/kufinyanga sarufi ili kutosheleza urari wa vina mf. maksudi yangu ngaliandaa
c) Ningetumia miti iliyofinda na yenye umbo nzuri/kutengenezea kijiti kwenye tundu la wimbombo/kupekechea moto kwa ufundi mkuukiwambono/ningekuwa fundi stadi katika upekechaji wa moto.
Tanbihi- wimbombo ni kipande cha mti kilichotobolewa tundu na kinachotumiwa kupekechea moto. Ulindi ni kijiti kinachopekechwa kwenye wimbombo ili kutoa moto.
d) Toni ya huzuni/ya kuomboleza/ya masikitiko
Mshairi anahuzunishwa na analalamikia hali yake ya upofu isiyomruhusu kujifanyia mambo mengi.
e)
? Urudiaji wa sauti mf. ubeti wa 1 – msatri wa mwisho kila ubeti
? Urudiaji wa silabi ra ra ra /a, a, a, /ngu, ngu, ngu n.k
? Urudiaji wa maneno ulo- ubeti wa 3, mato ubeti wa 1, 9
? Usambamba/urudiaji wa vishazi/urudiaji wa miundo sawa ya mistari mf. ngalifinyanga chungu, cha mduwaa.
f) Kipofu/mtu asiyeona. Ubeti wa 1 anasema, ngakua na mato.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 10:49
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho kamwe...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho kamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.
Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.
Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.
Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.
a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
c) Eleza toni ya shairi hili.
d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili?
e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande.
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi za maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
kumpapasa,kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha …
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani
katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama si kujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laiti angalijua!
(T. Arege)
Maswali
a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.
c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili.
d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:
i. tashhisi
ii. kinaya
iii. tashbihi
f) Eleza toni ya shairi hili.
g) Bainisha nafsineni katika shairi hili.
h) Changanua muundo wa shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
Ile sauti zamani kidogo
“Kuwa tayari kupanda na kushuka.”
Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima nifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka
Jambo moja nakukumbukia: Mungu
Je, nimwombe tena? Hadi lini?
Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!
Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
(a) Eleza toni ya shairi hili.
(b) Tambua nafsineni katika shairi hili.
(c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti wa tatu?
(d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka.
(e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
(f) Eleza maana ya:
(i) kuruba
(ii) barabara yenye ukungu
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami...(Solved)
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami imani, wala kupanga siasa
Mwasema sayansini, siku ningalitosa
Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika
Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza
Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao
Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia
Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote
Msamiati huwa, ni wa Afrika yote
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha
Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.
Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana
Kukua imeridhia, msamiati kufana
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana
Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia.
Maswali
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu
(b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu.
(f) Bainisha nafsineni katika shairi.
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
i. nasongwa
ii. kuriaria
iii. adinasi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana,...(Solved)
Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
(Abdalla Said Kizere)
Maswali
a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
d) Eleza umbo la shairi hili.
e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi (Solved)
Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi(Solved)
Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi(Solved)
Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema...(Solved)
Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Taja majina yanayopendekezwa
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi(Solved)
Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi(Solved)
Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi(Solved)
Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi(Solved)
Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
a) Sakarani
b) Ngonjera
c) Malumbano
d) Masivina
e) Taabili
f) Mandhuma
g) Kisarambe
h) Mavue
i) Sabilia
j) Togoo
k) Kumbukizi(Solved)
Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
a) Sakarani
b) Ngonjera
c) Malumbano
d) Masivina
e) Taabili
f) Mandhuma
g) Kisarambe
h) Mavue
i) Sabilia
j) Togoo
k) Kumbukizi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani(Solved)
Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno(Solved)
Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza aina za mashairi kulingana na vina(Solved)
Eleza aina za mashairi kulingana na vina
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo(Solved)
Eleza aina za mashairi kulingana na idadi ya vipande katika mshororo
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti (Solved)
Taja aina ya mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika ubeti
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.(Solved)
Uainisho wa bahari za mashairi hutegemea pakubwa vigezo mbalimbali. Taja vigezo hivyo.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)