a)
? Shairi hili ni wasia kwa vijana; unawaonya dhidi ya kushiriki mapenzi.
? Linashauri kuwa wanaovutia machoni wanaugua na hivyo wanaweza kuwaambukiza maradhi yasiyotibika.
? Zinaa hii haichagui wala kupendelea yeyote. Hata wenye nguvu au warembo wamesalimu amri. (ubeti 4)
? Vijana wajikaze kuhakikisha kuwa hawaingii kwenye mtego wa kushiriki mapenzi.
? Wapo watakaowasema wenye kujitunza lakini hilo lisiwafanye kutetereka.
b)
? Tabdila- kubadili miendelezo ya maneno pasi na kubadili idadi ya mizani. Mf. nisikia badala ya nisikie. Limetumiwa hivi ili kukidhi mahitaji ya vina.
? Inkisari- kufupisha maneno. Imetumiwa ili kuleta ulinganifu wa mizani. Mf. sikuwambia- sikuwaambia, jepusheni- jiepusheni, ngawa- ingawa, waone- uwaone, ngia- ingia, walopapia- waliopapia, watalokwambawatakalokwamba.
? Kuboronga sarufi/miundo ngeu ya kisintaksia- ni mpangilio wa maneno katika tungo kutofuata utaratibu wa kisarufi wa lugha ya Kiswahili. Mf. yaugua nisikia- nisikie yaugua, si mlango nyumba nzuri- nyumba nzuri si mlango, makaa kujipalia- kujipalia makaa, madhara kukadiriakukadiria madhara, mapoda kumichia- kumichia mapoda.
? Mazida- vyang’aria badala ya vyang’ara.
? Utohozi- Sitoria- history
Mazida na utohozi zimetumiwa kuleta urari wa vina.
c) Pande mbili ambazo mshairi anasema nazo ni;
? Vijana
? Mungu
d)
? Hutumiwa kusisitiza wazo au kumfanya msomaji kushawishika na mtazamo wa msanii. Kwa mfano ubeti wa 6, mshairi anamshawishi msomaji kwamba hakuna faida ya kuingilia anasa.
? Hutumiwa kuzindua. Ubeti wa 5 anamzindua msomaji kuona kuwa hata wenye nguvu huangamizwa na zinaa.
? Humfanya msomaji kulidadisi jambo linaloibuliwa. Katika ubeti wa sita msomaji atavuta fikra kuhusu ‘faida’ ya kuingia kwenye anasa ya kumuua. Kwa kulidadisi hili ataona kuwa hamna faida na hivyo kujirudi.
? Hutumiwa kusuta watu au kukashifu jambo. Ubeti wa 5 unawakashifu waliopapia anasa na kuwatahadharisha wasomaji kwa kuonyesha kuwa hatima ya anasa ni kifo.
? Maswali ya balagha ambayo yanalenga msomaji wa kazi ya fasihi hunuiwa kumfanya kulitafakari jambo hivyo kujifunza kwalo.
e)
? Toni ya huzuni/kusikitika- anasikitikia madhara yatakayowapata wanaoingilia zinaa kwa kauli kama vile ‘wawapi leo madume, anasa walopapia?’ ubeti 5
? Toni ya kunasihi au kushawishi- anawasihi vijana kuepuka zinaa. Mf anawaambia, ‘kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia.’ Ubeti 7
? Kukejeli/kudharau/stihizai/bezo
? Uchungu- anaonea uchungu tabia ya vijana.
francis1897 answered the question on February 1, 2023 at 11:05
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,
Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana,
Kiwa ni riziki yangu,...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,
Nikaiga rika langu, kwa vileo, na mbio za wsichana,
Kiwa ni riziki yangu, mapokeo, kuoa na kuona,
Ni wakati utanena.
Nashukuru kwa ugumba, wenye ndimi, wanipazao nao,
Wapitao wakiimba, eti mimi, ningapenda hali zao,
Haupandiki mgomba, wana nyemi, fisadi wa hadhi zao,
Eti ni kwa raha zao.
Ni lipi lenye kukera, kwa Muumbi, marufuku kwenye misa,
Ni mtu kuwa hawara, wa vitimbi, ama alozawa tasa?
Ugumba na ukapera, sio dhambi, wala haujawa kosa,
Waama sina makosa
Bora tungeni vitabu, magazeti, mutangaze kwa rediyo,
Muwaite watribu, kina Siti, watuzwa ilimu hiyo,
Na zaidi muhutubu, kwa umati, muwambe ambayo siyo,
Kwalo sichafuki moyo
Hidhuru yote ni bure, sio kitu, kudhiki asodhikika,
Siwi nikaona ghere, lailatu, nyota njema itafika,
Kwa shangwe na njerejere, kila mtu, mdomo utafumuka,
Akiri amejibika.
(Mwalaa M. Nyanje)
(a) Eleza jambo ambalo mzungumzaji (nafsineni) katika shairi hili anasingiziwa.
(b) Fafanua mambo matano ambayo mzungumzaji (nafsineni) anapinga katika shairi hili.
(c) Eleza umuhimu wa viishio vya beti za shairi hili.
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(e) Eleza muundo wa shairi hili.
(f) Bainisha matumizi mawili ya tafsida katika shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Watafuta Riziki
1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini
Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
Vyakula washakiki, visipungue vinyuani.
2. Watafuta riziki, wahaingaikao...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Watafuta Riziki
1. Watafuta riziki, watatokwa jasho vijijini
Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
Vyakula washakiki, visipungue vinyuani.
2. Watafuta riziki, wahaingaikao mijini
Kutwa kile na hiki, kama watanga na mipini
Japo hawasikii, hawakosi kujiamini
3. Watafuta riziki, wazalendo wa nchi hii
Kamwe hawajidhiki, tama za moyo kutii
Bali huafiki, kupingana na ulaghai
4. Watafuta riziki, pato ambalo la halali
Ndoto haizimiki, ya kesho kuwa njema hali
Wiki baada wiki, la haramu jasho hawali
(a) Fafanua sifa tano za watu wanaozungumziwa katika shairi hili.
(b) Bainisha umuhimu wa tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili.
(c) Eleza kwa kutoa mifano, mbinu tatu ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi.
(d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
(i) idadi ya mishororo katika beti.
(ii) mpangilio wa vina
(iii) mpangilio wa maneno
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza
1 Ngakua na mato, ya kuonea
Ngalisana kito,cha kuchezea
Kilicho kizito, cha kuelea
Kikamuenea,...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Amiri A. S. Andanenga: Sauti ya Kiza
1 Ngakua na mato, ya kuonea
Ngalisana kito,cha kuchezea
Kilicho kizito, cha kuelea
Kikamuenea, akivae.
2 Makusudi yangu,ngaliandaa
Ngafinyanga chungu, cha mduwaa
Ngatia vitangu,vinavong’aa
Ili ziwe taa, kwa apikae.
3 Mkungu wa tano, wa mduwara
Ulo bora mno, kisha imara
Ulo na maono, kuwa ni dira
Kwenye barabara, itindiae.
4 Ngaomba Baraka, kwake Rabana
Punje za nafaka, kila aina
Chunguni kuweka, kwa kulingana
Hajaangu suna, yule alae.
5 Ngafanya bidii, kwenda mwituni
Sio kutalii, kukata kuni
Ya miti mitii, huko jikoni
Isio na kani,ni iwakae.
6 Kwa yangu mabega, nikathubutu
Ngabeba mafiga, yalo matatu
Bila hata woga, kwenye misitu
Simba tembo chatu, sinitishie.
7 Miti yenye pindi,na jema umbo
Ngajenga ulindi, mwema wimbombo
Fundi aso fundi, penye kiwambo
Moyo wenye tambo, apekechae.
8 Singaajiri, ngachimba mimi
Kisima kizuri, cha chemchemi
Maji ya fahari, ya uzizimi
Jua la ukami, siyaishae
9 Tamati nafunga, kwa kuishia
Mato ndo malenga, kanikimbia
Nahofu kutunga, mabeti mia
Asije chukia, ayasomae.
(a) Eleza ujumbe wa shairi hili.
(b) Kwa kurejelea ubeti wa pili, eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi aliotumia mshairi.
(c) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Fafanua aina tatu za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili.
(f) Bainisha nafsi neni katika shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho kamwe...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho kamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.
Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.
Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.
Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.
a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
b) Fafanua mbinu nne za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
c) Eleza toni ya shairi hili.
d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili?
e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande.
f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza
Videge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihi za maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
kumpapasa,kumtoa matongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha …
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
Furaha ya mtu ni furaha gani
katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama si kujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laiti angalijua!
(T. Arege)
Maswali
a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili.
b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.
c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili.
d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.
e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:
i. tashhisi
ii. kinaya
iii. tashbihi
f) Eleza toni ya shairi hili.
g) Bainisha nafsineni katika shairi hili.
h) Changanua muundo wa shairi hili.
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruba
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
Ile sauti zamani kidogo
“Kuwa tayari kupanda na kushuka.”
Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima nifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka
Jambo moja nakukumbukia: Mungu
Je, nimwombe tena? Hadi lini?
Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!
Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendelee kujitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
(a) Eleza toni ya shairi hili.
(b) Tambua nafsineni katika shairi hili.
(c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti wa tatu?
(d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka.
(e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
(f) Eleza maana ya:
(i) kuruba
(ii) barabara yenye ukungu
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami...(Solved)
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia,nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami imani, wala kupanga siasa
Mwasema sayansini, siku ningalitosa
Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika
Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
Mzaliwapo mwalia, ‘maa’, maneno ya kwanza
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza
Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao
Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
Enyi viongozi wetu, ipangeni nadharia
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata ‘mbusha watu, tuche kuriaria
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia
Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote
Msamiati huwa, ni wa Afrika yote
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao ‘meomba kiasi, ili kujizidisha
Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.
Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana
Kukua imeridhia, msamiati kufana
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana
Lugha yetu ya maana, mwaipuuza yalia.
Maswali
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu
(b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hililikaitwa kilio cha lugha.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatu.
(f) Bainisha nafsineni katika shairi.
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
i. nasongwa
ii. kuriaria
iii. adinasi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana,...(Solved)
Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,
Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,
Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Dunia ingetatana, na kizazi katikati,
Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,
Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,
Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,
Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,
Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti
Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,
Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,
Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,
Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,
Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Peleleza utaona, hayataki utafiti,
Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,
Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,
Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,
Yote tuloelezana, katenda bila senti,
Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?
(Abdalla Said Kizere)
Maswali
a) Pendekeza anwani mwafaka la shairi hili.
b) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza
c) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi.
d) Eleza umbo la shairi hili.
e) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano.
f) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi.
g) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi (Solved)
Eleza mambo yanayozingatiwa katika uhuru wa kishairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi(Solved)
Taja baadhi ya masuala muhimu katika uchambuzi wa mashairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi(Solved)
Taja aina mbalimbali za takriri katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema...(Solved)
Katika ikisiri yake, Joseph Nyehita anaangazia kuwa matumizi ya methali yanapozingatiwa, ushairi wa Kiswahili unaweza kuainishwa zaidi kwa kuzingatia kutumiwa au kutotumiwa kwa methali. Anasema kuwa kila kikundi cha ushairi kinaweza kupendekezewa jina mahususi kuwa kitambulisho chake. Taja majina yanayopendekezwa
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi(Solved)
Taja huku ukitoa mfano, aina kadha za taswira katika ushairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi(Solved)
Taja na ueleze tamathali tofauti za usemi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi(Solved)
Taja mambo ya kuzingatia katika kueleza muundo wa shairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi(Solved)
Taja na ueleze mambo muhimu yanayozingatiwa katika uchambuzi wa mashairi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
a) Sakarani
b) Ngonjera
c) Malumbano
d) Masivina
e) Taabili
f) Mandhuma
g) Kisarambe
h) Mavue
i) Sabilia
j) Togoo
k) Kumbukizi(Solved)
Eleza aina za bahari za ushairi zifuatazo:
a) Sakarani
b) Ngonjera
c) Malumbano
d) Masivina
e) Taabili
f) Mandhuma
g) Kisarambe
h) Mavue
i) Sabilia
j) Togoo
k) Kumbukizi
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani(Solved)
Taja na ueleze aina za mashairi kulingana na mizani
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno(Solved)
Eleza aina ya mashairi kulingana na mpangilio wa maneno
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)
- Eleza aina za mashairi kulingana na vina(Solved)
Eleza aina za mashairi kulingana na vina
Date posted: February 1, 2023. Answers (1)