“Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala...

      

“Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala katika dondoo hili?
(c) Fafanua kilichokuwa kimetukia kabla ya dondoo hili.
d) Taja sifa mbili za mamake Umulkheri. (Naomi)

  

Answers


Francis
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
? Ni maneno ya Umu akijisaili kimoyomoyo
? Anajiuliza maswali haya baada ya askari mmoja kumuuliza swali
? Yupo katika kituo cha polisi
? Ameenda kupiga ripoti baada ya kupotea kwa ndugu zake wawili, Dick na Mwaliko

(b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala katika dondoo hili?
? Maswali balagha
? Mjadala nafsi – Umu anajiuliza haya maswali kimoyomoyo.

(c) Fafanua kilichokuwa kimetukia kabla ya dondoo hili.
? Naomi, mamake Umu, anamwandikia mumewe (Lunga) ujumbe mfupi wa simu kuwa ameondoka. Amechoshwa na ufukara wa mumewe.
? Lunga anajukumika kuwalinda wanawe kama baba na mama baada ya mkewe kumsaliti na kumwacha.
? Lunga anaaga dunia kutokana na uwele wa shinikizo la damu na kuwaacha wanawe mikononi mwa kijakazi wao Sauna.

d) Taja sifa mbili za mamake Umulkheri. (Naomi)
? Msaliti – anamsaliti mumewe na kumwacha wakati alipomhitaji zaidi kwa sababu ya umaskini wake.
? Asiyejali – hajali maslahi ya wanawe ambao wana umri mdogo. Anaondoka bila kujali nani atawatunza.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 05:14


Next: “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri)(a) Weka dondoo hili katika muktadha...
Previous: Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions