Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.

      

Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.

  

Answers


Francis
- Kuna matumizi ya vipera vya utanzu wa semi kama vile methali, misemo, nahau n.k. Mwandishi ametumia methali kutoa mafunzo mbalimbali na kuipamba riwaya. Kuna matumizi ya lakabu kwa mfano Dede.
- Kuna vipera vya mazungumzo kama vile hotuba. Mfano ni hotuba ya Lunga kwa wanafunzi wenzake shuleni. Hotuba yake inahusu uhifadhi wa mazingira. (uk 68) Hotuba nyingine ni ya Rechel Apondi akiwahutubia maafisa wa usalama kuhusu suala la usalama. (uk. 112)
- Mwandishi pia ametumia ushairi simulizi. Hapa kwa mfano kuna wimbo wa Shamsi unaozungumzia maswala mengi yanayowakumba kama vile unyakuzi wa ardhi, mishahara duni, unyanyasaji, mapendeleo katika kutoa nafasi za kazi, dawa kukosekana hospitalini, umaskini n.k (uk 129) Aidha kuna wimbo wa mbolezi wakati wa kuigiza kifo cha Dede. (uk. 60)
- Hali kadhalika, utanzu wa maigizo umetumika. Ndugu zake Dede wanaigiza kivigha kilichoambatana na mazishi ya Dede. (uk 59) Vilevile kuna maigizo ya mazungumzo akilini mwa Ridhaa kati yake na bintiye Annatila. (uk. 38)
- Mwandishi pia ameshirikisha utanzu wa hadithi/masimulizi katika riwaya. Wahusika kama vile Pete na Tuama wanasimulia visa vya maisha yao. (uk. 141) Vilevile kuna masimulizi ya maisha ya wanafunzi wenza wa Umu (Kairu, Mwanaheri, Zohali na Chandachema) katika shule ya Tangamano na hali iliyowapelekea kuwa katika shule hiyo.
(uk. 91-108)
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 05:17


Next: “Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala...
Previous: Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions