Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.

      

Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.

  

Answers


Francis
- Maisha ya Lunga na familia yake yanabadilika baada ya kurudishwa Mlima wa Simba. Naomi anashindwa kustahimili mabadiliko haya na anaondoka akimwachia mumewe kihoro cha upweke.
- Baada ya Umu kupata hifadhi kwa Mwangeka na Apondi, maisha yake yanachukua mkondo mpya, yanabadilika. Anahisi kama lile pengo lililoachwa na wazazi wake limejazwa, anasoma na anahitimu kama mhandisi.
- Maisha ya wahafidhina yanachukua mkondo mpya baada ya uchaguzi na kutawazwa kwa kiongozi mpya – Mwekevu. Vita vinazuka, watu wanauawa, mali inaharibiwa na wengi kufurushwa makwao na kufanywa wakimbizi katika Msitu wa Mamba.
- Kuna mabadiliko ya utawala/uongozi. Kwa kipindi kirefu mwanamume ndiye amekuwa akitawala ila sasa kiongozi mwanamke anapigiwa kura na kuchukua hatamu za uongozi.
- Taifa la wahafidhina pia limepiga hatua za kimaendeleo kutokana na mazungumzo ya Ridhaa na Tila. Hali ya maisha ni nafuu kama vile wahasiriwa wa Ukimwi wanapata dawa za bei nafuu za kuwawezesha kudhibiti makali ya ugonjwa huu, serikali pia imeanzisha elimu bila malipo.
- Kuangamizwa kwa familia ya Ridhaa katika mkasa wa moto kunabadilisha maisha yake kuwa ya simanzi na kilio.
- Hatua ya mkoloni kupuuza sera ya umiliki na matumizi ya ardhi inabadilisha maisha na mshikamano wa kijamii. Zamani ardhi ilimilikiwa na jamii nzima, sasa kila mtu anamiliki kipande chake cha ardhi na ana hatimiliki yake.
- Kutokana na ukubwa wa familia yake mzee Mwimo Msubili, anawahamishia wake wake wawili sehemu ya Msitu wa Heri. Maisha ya Ridhaa yanachukua mkondo mpya kwa kubaguliwa na wenzake nusra aache masomo.
- Kuna mabadiliko yanayofanyika shuleni kwa kina Ridhaa baada ya mamake kuzungumza na mwalimu wao kuhusu umuhimu wa kuwajuza wanafunzi umuhimu wa ushirikiano na kuishi kwa umoja. Ridhaa sasa anakumbatia masomo na kupaa katika anga za elimu na kuhitimu chuo kikuu.
- Ridhaa anabadilisha mazingira ya Msitu wa Heri, eneo ambalo lilijulikana kama Kalaharu (kutokana na ukavu) sasa likatwaa sura mpya ya chanikiwiti. Anapanda miti mingi inayoleta mvua na anahakikisha wanakijiji wanapata maji ya mabomba.
- Maisha ya Umu yanachukua mkondo mpya baada ya wanuna wake (Dick na Mwaliko) kutekwa nyara na Sauna. Anaishi bila makao hadi anapookolewa na Hazina.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 05:33


Next: Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.
Previous: “Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii. (c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions