Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii. (c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji...

      

“Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii.
(c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji na wakimbizi wengine katika kambi ya wakimbizi.

  

Answers


Francis
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
- Nafsineni ni Ridhaa.
- Anamwuliza shemeji/mwamu wake Kaizari.
- Wapo katika kambi ya wakimbizi katika Msiti wa Mamba.
- Wanajipata hapa baada ya kufurushwa makwao baada ya vita kuzuka baada ya kutawazwa kwa Mwekevu – kiongozi mwanamke.


(b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii.
- Msomi – amesoma hadi akafuzu kuwa daktari.
- Mvumilivu – anavumilia hali ya ukiwa baada ya kuchomewa familia na hata mali yake. Anavumilia vilevile hali mbaya ya mle kambini.


(c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji na wakimbizi wengine katika kambi ya wakimbizi.
- Walikumbwa na njaa. ‘...tulikula mate kutokana na ule ugeni wa kutojua hata kuliko na matunda mwitu.’ (uk. 27)
- Msongamano wa watu kwenye kambi hiyo.’ ...idadi yetu iliongezeka.’ (uk. 27)
- Baridi kali ya usiku. ‘...hali ya uhitaji ilitutuma kutafuta jinsi ya kujikinga na baridi ...’ (uk. 27)
- Walikosa maji safi ya kunywa. ‘Changamoto kubwa ilikuwa maji safi ya kunywa.’ (uk. 27)
- Makazi duni na chache. ‘Vijumba vichache tulivyovijenga havikutosha kuhimili idadi ya watu...’ (uk. 28)
- Ukosefu wa vyoo/mahali pa kwenda haja. ‘Ukosefu wa misala ulipelekea kuzaliwa kwa vyoo vya kupeperushwa...’
- Magonjwa yalianza kuenea kwa mfano ugonjwa wa kipindupindu kutokana na ukosefu wa misala. (uk. 29)
- Vifo vya watoto wao kutokana na kubwakurwa na magarimoshi walipojaribu kujijengea misala katikati mwa reli.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 05:37


Next: Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.
Previous: “Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri) (a) Eleza muktadha wa...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions