“Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri) (a) Eleza muktadha wa...

      

“Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza masaibu yaliyomkumba baba anayerejelewa maishani mwake.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
- Huu ni uzungumzi nafsi wa Mwangeka.
- Anamrejelea babake Ridhaa.
- Ni katika kiwanja cha ndege.
- Baada ya Mwangeka kumwona babake alipokuwa anarudi kutoka ziara ya kazi ya kudumisha amani katika nchi jirani.


(b) Eleza masaibu yaliyomkumba baba anayerejelewa maishani mwake.
- Familia yake iliteketea katika mkasa wa moto.
- Nyumba yake pia iliteketezwa moto.
- Nyumba zake zingine zilibomolewa kwa madai eti zilijengwa katika hifadhi ya barabara.
- Alikuwa mkimbizi katika Msitu wa Mamba na huko alikumbana na changamoto nyingi.
- Aliishi kwa upweke baada ya mke wake na aila yake kuangamia.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 05:39


Next: “Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii. (c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji...
Previous: “Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions