“Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa...

      

“Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa fimbo!”
(a) Weka maneno haya katika muktadha wake.
(b) Fafanua masuala mengine saba aliyowasilisha mzungumzaji.
(c) Kwa kurejelea sehemu nyinginezo za riwaya, jadili sifa zozote nne za mzungumzaji wa dondoo hili.

  

Answers


Francis
(a) Weka maneno haya katika muktadha wake.
- Ni maneno ya Rechel Apondi katika hotuba yake.
- Anawahutubia maafisa wa usalama.
- Ni katika ukumbi kulikoandaliwa warsha hiyo na Shirika la Msalaba Mwekundu.
- Hotuba inahusu jukumu la vikosi vya askari katika kudumisha usalama, amani na maridhiano nchini.


(b) Fafanua masuala mengine saba aliyowasilisha mzungumzaji.
- Alizungumzia umuhimu na jukumu la kila mtu kudumisha amani, siyo askari pekee.
- Vikosi vya askari na wanajeshi wana ujuzi wa njia mwafaka za kutatua migogoro na kupalilia maridhiano.
- Raia wanahitaji zaidi ushauri badala ya vipigo.
- Aliwatahadharisha kuhusu vilio vya raia kwa kile wanachokiita extra judicial killings yaani mauaji ya raia kwa kutumia nguvu.
- Aliwaonya walinda usalama dhidi ya kutaahiri/kuchelewa kufika pahali palipotokea mkasa – utepetevu kazini/kuzembea kazini kwani hili huchangia vifo ambavyo vingezuiliwa.
- Aliwataka maafisa wajitenge na njama za kifisadi na nyendo nyingine hasi.
- Alizungumzia pia suala la maafisa wa askari kushindwa kudhibiti hasira zao hivyo kufyatua risasi ovyoovyo na kusababisha vifo haswa kwa vijana.
- Aliwakumbusha kuwa hata wahalifu wana haki, kwa mfano ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kabla hawajapewa adhabu yoyote.


(c) Kwa kurejelea sehemu nyinginezo za riwaya, jadili sifa zozote nne za mzungumzaji wa dondoo hili.
- Ni msomi - Apondi ana shahada katika taaluma ya masuala ya kijamii.
- Jasiri – Mwangeka anamtaja Apondi kama mtu jasiri baada ya kutoa hotuba yake.
- Mshauri – anawashauri maafisa wa polisi na wanajeshi kuhusu namna ya kudumisha amani, usalama na maridhiano.
- Mkarimu/ana moyo mkunjufu – kupitia kwake, Umu anakuwa mtoto wa kupanga katika familia hii. Kuzaliwa kwa Umulkheri katika familia ya Apondi na Mwangeka kulikuwa zao la ukarimu wao. (uk 116)
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 05:44


Next: “Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri) (a) Eleza muktadha wa...
Previous: “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri) (a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu. (b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions