“Kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati. Bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Nisingepashwa tohara nisingeolewa. Msiba uliowapata wenzangu ni bahati mbaya tu.” (Chozi la...

      

“Kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati. Bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Nisingepashwa tohara nisingeolewa. Msiba uliowapata wenzangu ni bahati mbaya tu.” (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.
(c) Taja mbinu ya sanaa iliyotumika katika dondoo hili.
(d) Jadili hulka moja ya msemaji wa dondoo hili kwa kurejelea dondoo.
(e) Eleza kinyume cha kauli ya nafsineni kwa kurejelea hoja tano kutoka kwenye riwaya.

  

Answers


Francis
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
- Anayesema maneno haya ni Tuama.
- Anawaambia Selume na Meko (wauguzi katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya)
- Yupo kitandani amelazwa katika kituo hicho.
- Tuama amelazwa kutokana na kupashwa tohara, jambo lililomuathiri kiafya na kumpelekea kupoteza damu nyingi.


(b) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.
- Mila potovu za jamii – jamii ya Tuama ingali inaamini katika mila zilizopitwa na wakati. Tuama na wasichana wenzake katika jamii yao wanapashwa tohara, suala linalowaathiri kwa njia nyingi. Tuama anadai eti asingepashwa tohara asingeolewa, na kwamba mwanamke ambaye hajapashwa tohara anabaki kuwa mtoto. Upashwaji tohara wa wanawake ni mila potovu iliyopitwa na wakati.


(c) Taja mbinu ya sanaa iliyotumika katika dondoo hili.
- Kinaya – Tuama anasema kuwa msiba uliowapata wenzake baada ya kupashwa tohara ni bahati mbaya ilhali naye pia amefikwa na msiba kutokana na upashaji tohara hadi akalazwa hospitalini.
- Ni kinaya Tuama (mwanamke) kuunga mkono upashaji tohara badala ya kuwa katika mstari wa mbele kuupinga huku anafahamu madhara yake.


(d) Jadili hulka moja ya msemaji wa dondoo hili kwa kurejelea dondoo.
- Ni mhafidhina – mhafidhina ni mtu ambaye hushikilia dini, mila na tamaduni za kale na akakataa kubadilika. Tuama angali anashikilia mila za jamii yake kuhusu upashaji tohara. Hayuko tayari kubadilika na kuasi mila hizo.


(e) Eleza kinyume cha kauli ya nafsineni kwa kurejelea hoja tano kutoka kwenye riwaya. Hakika si kweli anavyodai Tuama kuwa kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati na eti msiba uliowapata wenzake ni bahati mbaya tu kwa sababu:
- Tohara huweza kusababisha kifo kama anavyosema muuguzi Meko. Wenzake Tuama wanapukutika wakati ambao jamii yao inawahitaji mno.
- Tohara huweza kusababisha wasichana kuacha masomo yao hivyo kuwahini nafasi za kazi baadaye na kuchangia katika maendeleo ya kitaifa.
- Huweza kuchangia ndoa za mapema baada ya wasichana kupashwa tohara.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:00


Next: “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri) (a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu. (b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama...
Previous: “Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali....

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions