(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
- Anayesema maneno haya ni Tuama.
- Anawaambia Selume na Meko (wauguzi katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya)
- Yupo kitandani amelazwa katika kituo hicho.
- Tuama amelazwa kutokana na kupashwa tohara, jambo lililomuathiri kiafya na kumpelekea kupoteza damu nyingi.
(b) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.
- Mila potovu za jamii – jamii ya Tuama ingali inaamini katika mila zilizopitwa na wakati. Tuama na wasichana wenzake katika jamii yao wanapashwa tohara, suala linalowaathiri kwa njia nyingi. Tuama anadai eti asingepashwa tohara asingeolewa, na kwamba mwanamke ambaye hajapashwa tohara anabaki kuwa mtoto. Upashwaji tohara wa wanawake ni mila potovu iliyopitwa na wakati.
(c) Taja mbinu ya sanaa iliyotumika katika dondoo hili.
- Kinaya – Tuama anasema kuwa msiba uliowapata wenzake baada ya kupashwa tohara ni bahati mbaya ilhali naye pia amefikwa na msiba kutokana na upashaji tohara hadi akalazwa hospitalini.
- Ni kinaya Tuama (mwanamke) kuunga mkono upashaji tohara badala ya kuwa katika mstari wa mbele kuupinga huku anafahamu madhara yake.
(d) Jadili hulka moja ya msemaji wa dondoo hili kwa kurejelea dondoo.
- Ni mhafidhina – mhafidhina ni mtu ambaye hushikilia dini, mila na tamaduni za kale na akakataa kubadilika. Tuama angali anashikilia mila za jamii yake kuhusu upashaji tohara. Hayuko tayari kubadilika na kuasi mila hizo.
(e) Eleza kinyume cha kauli ya nafsineni kwa kurejelea hoja tano kutoka kwenye riwaya. Hakika si kweli anavyodai Tuama kuwa kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati na eti msiba uliowapata wenzake ni bahati mbaya tu kwa sababu:
- Tohara huweza kusababisha kifo kama anavyosema muuguzi Meko. Wenzake Tuama wanapukutika wakati ambao jamii yao inawahitaji mno.
- Tohara huweza kusababisha wasichana kuacha masomo yao hivyo kuwahini nafasi za kazi baadaye na kuchangia katika maendeleo ya kitaifa.
- Huweza kuchangia ndoa za mapema baada ya wasichana kupashwa tohara.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:00
- “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri)
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu.
(b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama...(Solved)
“Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri)
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu.
(b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama msemaji maishani.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa...(Solved)
“Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa fimbo!”
(a) Weka maneno haya katika muktadha wake.
(b) Fafanua masuala mengine saba aliyowasilisha mzungumzaji.
(c) Kwa kurejelea sehemu nyinginezo za riwaya, jadili sifa zozote nne za mzungumzaji wa dondoo hili.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa...(Solved)
“Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza masaibu yaliyomkumba baba anayerejelewa maishani mwake.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii.
(c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji...(Solved)
“Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii.
(c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji na wakimbizi wengine katika kambi ya wakimbizi.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.(Solved)
Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.(Solved)
Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala...(Solved)
“Sasa nitajuaje walichokuwa wamevalia nami sikuwaona? Mtu hukwambia anapotoroka au kutoroshwa?” (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Ni mbinu zipi za lugha zinazotawala katika dondoo hili?
(c) Fafanua kilichokuwa kimetukia kabla ya dondoo hili.
d) Taja sifa mbili za mamake Umulkheri. (Naomi)
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri)(a) Weka dondoo hili katika muktadha...(Solved)
1. “Huyu ambaye mama alimwona kuwa gae, kumbe sasa ndiye chombo cha kunivisha bahari hii ya dhiki?” (Chozi la Heri)
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake faafu.
(b) Eleza mbinu mbili za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.
(c) Eleza jinsi mrejelewa alivyomsaidia nafsineni.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza mbinu zifuatazo zilivyotumika kwenye hadithi, Pupa, ukitolea mifano;
i. Kinaya
ii. Sadfa(Solved)
Eleza mbinu zifuatazo zilivyotumika kwenye hadithi, Pupa, ukitolea mifano;
i. Kinaya
ii. Sadfa
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Umaskini na usherati ni baadhi ya mambo ambayo hudidimisha maendeleo. Thibitisha kauli hii ilivyotumika katika hadithi, Pupa.(Solved)
Umaskini na usherati ni baadhi ya mambo ambayo hudidimisha maendeleo. Thibitisha kauli hii ilivyotumika katika hadithi, Pupa.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Je, anwani Pupa inafaa? Fafanua.(Solved)
Je, anwani Pupa inafaa? Fafanua.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Huku ukitolea mifano, eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Nilitamani;
(i) Kinaya
(ii) Taharuki
(iii) Taswira(Solved)
Huku ukitolea mifano, eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Nilitamani;
(i) Kinaya
(ii) Taharuki
(iii) Taswira
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Mwandishi wa hadithi, Nipe Nafasi ameshughulikia vipi suala la ’ utamaduni na mabadiliko’(Solved)
Mwandishi wa hadithi, Nipe Nafasi ameshughulikia vipi suala la ’ utamaduni na mabadiliko’
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Taasubi ya Kiume na migogoro ni baadhi ya masuala makuu katika hadithi, Nipe Nafasi. Jadili.(Solved)
Taasubi ya Kiume na migogoro ni baadhi ya masuala makuu katika hadithi, Nipe Nafasi. Jadili.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Fafanua kwa kina masuala ibuka yafuatayo katika hadithi ya Toba ya Kalia;
(i) Elimu
(ii) Teknolojia na mawasiliano(Solved)
Fafanua kwa kina masuala ibuka yafuatayo katika hadithi ya Toba ya Kalia;
(i) Elimu
(ii) Teknolojia na mawasiliano
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Je, anwani, Toba ya Kalia inafaa? Eleza.(Solved)
Je, anwani, Toba ya Kalia inafaa? Eleza.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Fafanua masuala yafuatayo katika hadithi, Ahadi ni Deni;
(i) nafasi ya mwanamke katika jamii
(ii) Familia na Malezi(Solved)
Fafanua masuala yafuatayo katika hadithi, Ahadi ni Deni;
(i) nafasi ya mwanamke katika jamii
(ii) Familia na Malezi
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Kifo cha Suluhu;
(i) Kinaya
(ii) Barua(Solved)
Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika hadithi, Kifo cha Suluhu;
(i) Kinaya
(ii) Barua
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- “Mabadiliko ni mambo ya lazima katika jamii,” thibitisha kauli hii katika hadithi ya Kifo cha Suluhu.(Solved)
“Mabadiliko ni mambo ya lazima katika jamii,” thibitisha kauli hii katika hadithi ya Kifo cha Suluhu.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)
- Asasi ya ndoa imejaa thamani na msukosuko. Thibitisha kutumia hadithi ya Kifo cha Suluhu.(Solved)
Asasi ya ndoa imejaa thamani na msukosuko. Thibitisha kutumia hadithi ya Kifo cha Suluhu.
Date posted: January 30, 2023. Answers (1)