“Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali....

      

“Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali. Nimechoka kuongolewa kwa wimbo wa performance contract.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa nukuu hii.
(b) Thibitisha tamathali mbili za usemi zinazodhihirika katika dondoo hili.
(c) Maudhui gani yanayowasilishwa katika dondoo hili?
(d) Kwa mujibu wa riwaya, ni mambo yapi yanayomchosha mzungumzaji wa kauli hii.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa nukuu hii.
- Ni maneno ya Selume
- Anajisemea maneno haya
- Ni baada ya kukumbuka hali ilivyo katika hospitali za umma hapo awali akiwa muuguzi katika mojawapo ya hospitali za umma.


(b) Thibitisha tamathali mbili za usemi zinazodhihirika katika dondoo hili.
- Takriri – neno nimechoka limerudiwa.
- Kuchanganya ndimi – nimechoka kuongolewa kwa wimbo wa perfomance contract.
- Uzungumzi nafsi/mjadala nafsi/monolojia – haya ni maneno anayojisema Selume.


(c) Maudhui gani yanayowasilishwa katika dondoo hili?
- Ufisadi – dawa zilizotengewa hospitali zinaishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali.
- Ubinafsi – wasimamizi wananyakua shehena za dawa bila kujali maslahi ya wagonjwa. Wao wanajali maslahi yao tu na faida watakazopata wakiuza dawa hizi.
- Changamoto zinazokumba hospitali za umma/sekta ya afya – kuna changamoto anuwai kama vile wagonjwa kufa kwa kukosa huduma za kimsingi, kuna ufisadi katika hospitali hizi n.k.


(d) Kwa mujibu wa riwaya, ni mambo yapi yanayomchosha mzungumzaji wa kauli hii.
- Hakuna vifaa vya kimsingi vya kufanyia kazi katika hospitali kwa mfano glavu. (uk. 139)
- Ukosefu wa dawa za wagonjwa hasa kina mama wanaoenda kujifungua. (uk. 140)
- Umeme kukatwa kwa sababu usimamizi wa hospitali haujalipia gharama zake.
- Wagonjwa kufa kwa kukosa huduma za kimsingi.
- Ufisadi uliokithiri katika hospitali hizi.
- Ahadi zisizotimizwa kama vile kuimarisha kampeni dhidi ya polio, kujenga vituo vya ushauri kwa wagonjwa wa UKIMWI na saratani n.k.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:05


Next: “Kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati. Bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Nisingepashwa tohara nisingeolewa. Msiba uliowapata wenzangu ni bahati mbaya tu.” (Chozi la...
Previous: “Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions