“Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea...

      

“Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa
tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea kiweo hakikatwi.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa dondoo.
(b) Tambua tamathali ya lugha iliyotumika katika dondoo.
(c) Ni maudhui yapi yanayojitokeza katika dondoo hili?
(d) Fafanua sifa mbili za mzungumzaji wa kauli ya kwanza.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa dondoo.
? Kauli ya kwanza ni ya Tuama. Anamjibu Meko.
? Ni katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya
? Tuama amelazwa kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kupashwa tohara.
? Kauli ya pili ni maneno ya Selume. Anamwambia Tuama.

(b) Tambua tamathali ya lugha iliyotumika katika dondoo.
? Methali – mwana akinyea kiweo hakikatwi.

(c) Ni maudhui yapi yanayojitokeza katika dondoo hili?
? Usaliti – Tuama anamsaliti babake kwa kupashwa tohara ilhali babake, Mzee Maarifa ndiye muasisi wa kikundi cha kupigania haki za kibinadamu kijijini mwao.

(d) Fafanua sifa mbili za mzungumzaji wa kauli ya kwanza.
? Msaliti – anamsaliti babake na juhudi zake za kutetea haki za kibinadamu kwa kukubali kupashwa tohara.
? Mwepesi wa kushawishika – anashawishika na shinikizo la wenzake na anakubali kupashwa tohara.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:12


Next: “Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali....
Previous: Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions