Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.

      

Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.

  

Answers


Francis
? Ubakaji. Genge la mabarobaro watano lilifululiza hadi walipokuwa Lime na Mwanaheri na kuwatendea unyama huku baba yao akitazama bila uwezo wa kuwasaidia.
? Ulanguzi wa dawa za kulevya. Dick anafanya kazi ya kusafirisha dawa za kulevya kutoka nchi moja hadi nyingine, na hii ni biashara ambayo inafanywa na vijana wengi, na kuwafanya wengine kuingia kwenye mitego ya polisi na kuelekea kutumikia kifungo chao gerezani.
? Uporaji, wizi na ukatili. Nyumba na mali yote ya Ridhaa inateketezwa, wakiwemo watoto wake na mkewe pia. Pia, mali ya wananchi kama mashamba yananyakuliwa na wanaachwa bila chochote.
? Uendelezaji wa biashara haramu. Bi. Kangara walifanya biashara haramu ya kuwauza watoto na vijana.
? Uavyaji mimba. Sauna anapata mimba kiholela na kujaribu awezavyo kuiavya, na mwishowe, baada ya kushindwa kuavya mimba, anaamua kujiua.
? Mapenzi kati ya baba mlezi na bintiye. Babake Sauna anafanya mapenzi na mwanawe apatapo nafasi, na mwishowe, Sauna anapata mimba. Hili ni jambo ambalo halijakubalika katika jamii na pia ni jambo la kufadhaisha sana na lenye kuleta laana.
? Kutupwa kwa watoto wachanga. Haswa wasichana wadogo wanapopata mimba bila ya kujipanga, wakishindwa kuavya mimba, wanaelekea kukitupa kitoto hicho kichanga punde tu baada ya kujifungua. Neema anaokota mtoto aliyetupwa jaani.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:27


Next: “Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea...
Previous: “Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions