Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

      

“Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

  

Answers


Francis
Mabadiliko ni hali ambapo mambo yanaenda kinyume na jinsi yalivyokuwa yakienda mbeleni. Hali ya kufanya mambo inabadilika na kuwa tofauti ya kawaida yake.
? Mfumo uliokuwepo hapo awali wa kumiliki mashamba barani Afrika ulipigwa marufuku na kukawa na mfumo mpya wa umiliki wa mashamba uliohusisha kupewa kwa hatimiliki.
Haya ni mabadiliko yanayokuja katika jamii. Sera mpya ya umilikaji nafsi wa ardhi ilimaanisha kwamba wale waliokosa pesa za kununulia mashamba wangekosa mahali pa kuishi. Na hata wale waliobahatika kuwa na pesa za kununulia mashamba daima walichukuliwa kama wageni wasiopasa kuaminiwa.
? Kuna mabadiliko yanayofanyika katika shule baada ya mamake Ridhaa kuzungumza na mwalimu wake kuhusu umuhimu wa kuwajuza wanafunzi ushirikiano na kuishi kwa umoja. Mabadiliko haya yanakuwa ya maana sana kwa Ridhaa kwani elimu yake inaendelea kwa ufasaha na anahitimu hadi chuo kikuu.
? Eneo ambalo awali likiitwa Kalahari, sasa limetwaa rangi ya chanikiwiti. Miambakofi, mivule na miti mingine mingi imepandwa. Mvua inanyesha majira baada ya mengine. Haya ni mabadiliko yanayofanyika katika mtaa huu ambao ulikuwa hapo awali umekauka sana lakini baada ya maji ya mabomba kufikishiwa watu, tunapata kuwa kunabadilika na ile hali ya kuwa jangwa inaisha, miti mingi inapandwa na hata mvua nyingi kunyesha.
? Maisha ya Umu yalichukua mkondo mpya. Siku ile baada ya kuwapigia polisi ripoti, ilibainika kuwa wanuna wake walikuwa wametekwa nyara na Sauna.
? Maisha ya Ridhaa pia yanachukua mkondo mpya au kubadilika wakati familia yake inapoangamia kwenye janga la moto, na mali yake yote kuishia hapo. Maisha yaliyokuwa ya furaha pamoja na familia yake yanabadilika na kuwa uchungu mtupu na kilio cha kufiwa na wapenzi wake.
? Kumekuwa na mabadiliko mengi sana katika serikali na pia hali ya maisha ya raia, bila kusahau elimu. Katika ukurasa wa 40 tunasoma; “Ridhaa: Na nani akasema viongozi waliopo hawajajikuna wajipatapo?”
? Wahasiriwa wa magonjwa sugu kama vile iri na hata UKIMWI wana dawa za bei nafuu za kuwawezesha kudhibiti hali hizi.
? Serikali imeanzisha sera ya elimu bila malipo kwa shule zote za msingi.
? Serikali imegharamia karo za shule za kutwa katika shule za upili na kuanzisha mradi wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi kuanzia darasa la kwanza ana kipakatalishi chake.
? Msitu wa Mamba uligeuka na kuwa nyumbani mwa maelfu ya watu waliogura makwao bila tumaini la kurudi. Maduka na majumba yanajengwa, na ile hali ya kuwa msitu inabadilika, na mashamba ya watu ndiyo yanayoonekana kwa sasa.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:39


Next: Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.
Previous: Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions