Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.

      

Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.

  

Answers


Francis
Migogoro ni mivutano na mikinzano mbalimbali katika kazi ya fasihi. Migogoro huweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka tofauti, nyadhifa mbalimbali, kiuchumi, nafasi katika jamii au hata kisiasa. Aina za migogoro katika riwaya hii.
? Kuna mgogoro kwenye familia ya Mzee Mwimo Msubili, kwa sababu familia yake ilikuwa kubwa na hakuitosheleza kwa chakula. Uk 9, “Wingi wa vinywa vya kulishwa ulizua uhasama, migogoro na hata uhitaji mkubwa.”
? Mgogoro wa kijamii unajitokeza baada ya mkoloni kupuuza sera za Mwafrika. Hatua ya mkoloni ya kupuuza sera za Mwafrika za umiliki wa ardhi na kuamua kujumuisha pamoja ardhi iliyomilikiwa na mtu binafsi na kuidhinisha umiliki huu kwa hatimiliki, ilivuruga mshikamano wa kijamii.
? Panatokea mgogoro shuleni wakati Ridhaa aliitwa ‘mfuata mvua’, na kutengwa na wenzake. Walimwona kama mwizi. Uk 10, “Wewe ni mfuata mvua. Hatutaki kucheza nawe. Umekuja hapa kutushinda katika mitihani yote. Wewe ndiwe unayetuibia kalamu zetu.”
? Ridhaa alijipata katika hali ya mgogoro na nafsi yake. Miguu yake sasa ilianza kulalamika pole pole, parafujo za mwili wake zililegea... Baada ya muda wa mvutano wa hisia na mawazo, usingizi ulimwiba.
? Kuna mgogoro uliosababishwa na wanasiasa, juu ya nani atakayekuwa kiongozi wa jamii, kati ya mwanamke mwananume.
? Mgogoro mwingine ulijitokeza kati ya raia na polisi, wakiwa katika harakati zao za kuweka amani. Uk 19, “Mchezo wa polisi kukimbizana na raia ulianza. Katika mchezo huo mamia ya roho zisizo na hatia zilisalimu amri chini ya pambaja za risasi na mapigo ya rungu, vitoa machozi navyo vikafanya kazi barabara.”
? Nyamvula anajikuta katika mgogoro na nafsi yake, wakati ambapo imani yake inakinzana na kazi ya mumewe kuwa askari.
? Tila anaitaja migogoro kadha katika tamthilia ya Hussein. Tamthilia hii ya Mashetani inayorejelewa ina migogoro mingi sana kama: migogoro ya kisiasa, kiuchumi, na pia ya kijamii.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:41


Next: “Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.
Previous: Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions