Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.

      

Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.

  

Answers


Francis
Ndoa ni maafikiano rasmi baina ya mume na mke ili waweze kuishi pamoja.
? Kuna ndoa kati ya Ridhaa na Terry. “Baadaye Ridhaa aliamua kuasi ukapera, akapata mke, Terry.”
? Mwangeka alikutana na Lily Nyamvula katika Chuo kikuu na kumwoa. Walibarikiwa na mtoto mmoja kwa jina Becky. Ndoa hii haikudumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto.
? Baada ya ndoa ya mwanzo kusambaratika, Mwangeka alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa.
? Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema. Hawakujaliwa kupata mwana wao kindakindaki japo walipanga mwana kwa jina Mwaliko.
? Kangata alikuwa na mke wake kwa jina Ndarine. Walibarikiwa na wana wafuatao. Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri. Lucia Kiriri – Kangata alikuwa ameolewa katika ukoo wa Waombwe ambao awali walikuwa maadui sugu wa ukoo wa Anyamvua. Ndoa hii ilipata pingamizi sana kutoka kwa ukoo mzima lakini kutokana na msimamo imara wa Kangata ndoa hii ilisimama.
? Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira. Walibarikiwa na mabinti wawili, Lime na Mwanaheri.
? Lunga alikuwa na mke kwa jina Naomi. Walikuwa na wana watatu, Umu, Dick na Mwaliko. Ndoa hii haikudumu kwani Naomi alimwacha Lunga na kwenda mjini alikokuwa shangingi kwelikweli.
? Ndoa baina ya Pete na Fungo. Pete alipoingia darasa Ia saba alipashwa tohara nao wajombake wakapokea posa na baadaye mahari kutoka kwa buda mmoja kwa jina Fungo aliyemuoa kama mke wa nne. Ndoa hii haikudumu kwani Pete alihiari kumwacha Fungo.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:44


Next: Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.
Previous: Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions