Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.

      

Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.

  

Answers


Francis
? Ridhaa aliungana na vijana wengine kwenda shuleni kupata elimu. “Ridhaa alikuwa mmoja wa waathiriwa wa hali hii. Anakumbuka jinsi siku ya kwanza shuleni alivyotengwa na wenzake katika mchezo wao wa kuvuta, mchezo wa kusukuma vifuniko vya chupa ya soda kwa ncha za vidole vyao.”
? Ridhaa alipea kwenye anga za elimu, akabisha kwenye milango ya vyuo, akafika kilele cha ufanisi alipohitimu kama daktari.
? Mwaliko pia anaendeleza masomo yake hadi akafika chuo kikuu. Hata alipohitimu masomo yake ya kidato cha nne na kujiunga na chuo kikuu kusomea shahada ya Isimu na Lugha, Mwangemi na Neema walijua kuwa juhudi zao za malezi hazikuambulia patupu.
? Mwangeka anapatikana anaenda shuleni kupata Elimu. Tunaambiwa kuwa Jumamosi moja, Mwangeka alikuwa ametoka shuleni, na siku hizo walimu walikuwa wameng’ang’ania kuwafunza Jumamosi wanafunzi waliokaribia ‘ICU’, kama walivyoliita darasa la nane. Baadaye anaonekana kuendeleza masomo yake hadi chuo kikuu na kuajiriwa kazi.
? Lunga Kiriri Kangata anapata elimu yake, kwani tunapata kumuona kama amiri-jeshi wa uhifadhi wa mazingira walipokuwa shuleni. Tunaambiwa kuwa kila Ijumaa wakati wa gwaride, Lunga angehutubia wanafunzi wenzake na walimu kuhusu mazingira.
? Umulkheri anaenda kupata elimu yake katika shule. Tunampata mwalimu wake akijaribu kumrejesha Umu darasani wakati fikra zake zinapoondoka katika shughuli za masomo. Tunapata pia kuwa kwa hali ambayo Umu alikuwa akiishi, mwalimu mkuu wa Shule ya Tangamano, anamsajili kuwa mwanafunzi huko, kwa hisani yake na kwa ushauri wa wizara ya elimu (uk 78). Umulkheri anayaendeleza masomo yake hadi chuo kikuu, anapoenda ughaibuni kusomea huko (uk 128).
? Pete pia anatumika katika kuwasilisha maudhui ya elimu, ingawa elimu yake inagonga mwamba baada ya kuozwa kwa mzee mmoja alipokuwa katika darasa la saba.
? Baada ya Naomi kuhangaika kwa miaka mingi akiwatafuta watoto wake, anaamua kuanzisha biashara ndogo karibu na chuo kikuu cha Mbalamwezi, na kazi anayoifanya ni kuwapigia wasomi chapa na kuisarifu miswada yao. Kwa hivyo, tunapata kuwa maudhui haya ya elimu yanajitokeza pia, kwa kuwepo kwa chuo kikuu.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:49


Next: Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.
Previous: Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions