Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.

      

Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.

  

Answers


Francis
? Ridhaa alimpenda sana mkewe Terry na wanawe. “Polepole parafujo za mwili wake zililegea, akaketi juu ya majivu - la, juu ya miili ya wapenzi wake.”
? Kuna mapenzi kati ya Mwangeka na baba yake Ridhaa. Haya ni mapenzi ya mzazi kwa mwanawe, Ridhaa alimpenda sana mwanawe Mwangeka kwani ndiye pekee aliyenusurika mauti.
? Mapenzi yanajitokeza kati ya Billy na Sally. Sally alikuwa msichana ambaye Billy alichumbia kwao, na kisha akamleta katika nchi hii ya kiafrika ili kumuonyesha mahali wangeweza kuishi baada ya kufunga akida. Kwa bahati mbaya, Billy anasalitiwa na mpenzi wake Sally na kuambiwa kuwa jumba lenyewe ni kama kiota cha ndege, mahali ambapo yeye hawezi akaishi hata kuwe vipi.
? Kuna mapenzi kati ya Subira na wanawe Mwanaheri na Lime. Hili linajidhihirika baada ya Subira kumwandikia barua Mwanaheri. Haya ni mapenzi ya mzazi lakini Subira anawasaliti wanawe.
? Kuna mapenzi kati ya Umulkheri na wazazi wapya wa kupanga, Mwangeka na mkewe Apondi anaowapata baadaye. Mwangeka na Apondi wanampenda sana Umu na kusema kuwa ni baraka za Mungu za kumfidia mwana wao aliyeaga dunia. Umulkheri naye anawapenda sana hawa wazazi wake wapya kwani waliweza kumlipia karo. Pia waliweza kumponya uchungu aliokuwa nao moyoni wa kuachwa na wazazi wake.
? Kuna mapenzi yanayojidhihirika katika familia hii ya Mwangeka na Apondi, kwa wana wao. Wakati unapofika wa Umulkheri kwenda kuyaendeleza masomo yake ughaibuni, wanamsindikiza hadi kwenye uwanja wa ndege. Mapenzi makali yanajidhihirisha wakati kila mmoja wao analia machozi kwa kuachana na Umu alipokuwa akiliabiri ndege.
? Kuna mapenzi kati ya Mwaliko na wazazi wake wa kupanga ambao ni Mwangemi na Neema. Hawa wawili wanampenda sana Mwaliko, naye Mwaliko anawapenda kama wazazi wake.
? Naomi anawapenda sana wanawe ingawa alikuwa amewasaliti kwa kuwaacha wakiwa wachanga. Ameishi kuwatafuta walikopotelea kwa miaka mingi, lakini mwishowe, anawapata wanawe wakiwa hai na wamejiendeleza sana kimaisha na kimasomo. Anawaomba msamaha huku akiwa na uchungu mwingi rohoni mwake. Wanawe wanamsamehe mwishowe kwa mapenzi waliyokuwa nayo kwake.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 06:52


Next: Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.
Previous: Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions