Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

      

Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.

  

Answers


Francis
? Bibi anamwelezea Ridhaa kuwa unyonge haukuumbiwa ‘majimbi’ ambao ni wanaume, bali uliumbiwa ‘makoo’, yaani wanawake. Hivyo basi jamii iliwadhalilisha wanawake tangu zamani.
? Mzee mwenye wake na wana wengi alihesabiwa kuwa mkwasi kwelikweli. “...basi wake hawa hawakuchelea kutimiza amri ya maumbile, wakapania kuujaza ulimwengu.” Wanawake wanadhalilishwa kwa kuonekana kana kwamba jukumu lao kuu katika jamii ni kuijaza dunia. Mwanamke hapewi nyadhifa muhimu katika jamii ila tu kazi yake ni kuolewa na kujaaliwa na wana wengi awezavyo.
? Viongozi wengi wa awali walibwagwa chini na vijana chipukizi. La kuhuzunisha ni kwamba wengi walishindwa kabisa kukubali ushindi, hasa yule ambaye alikuwa anagombea kilele cha uongozi. Kulingana naye, nafasi hii iliumbiwa mwanamume, na kupewa mwanamke ni maonevu yasiyovumilika. “Katika hali hii, jamii haikukubali wanawake kuwa viongozi, bali cheo hiki cha uongozi kilikuwa cha jinsia ya kiume.”
? Msichana anaonekana kutokuwa na umuhimu wa kupelekwa shuleni ili kupata elimu, ilhali yeye mwenyewe anaazimia kuendeleza masomo yake. Maazimio ya Pete kupata elimu yanagonga mwamba baada ya kuozwa kwa mzee Fungo ambaye anamtesa na mwishowe kumtaliki na kitoto kichanga.
? Mamake Sauna hana uhuru wa kuzungumza kwake, wala kuuliza maswali, na iwapo ameuliza swali, inakuwa ni vita au kichapo kutoka kwa mumewe.
? Sauna anadhalilishwa kwa kubakwa na babake mzazi, wala sio mara moja. Hatimaye anapata mimba ya babake mzazi. Jambo hili linamdhalilisha sana Sauna hivi kwamba heshima yake yote inapotea, na hawezi kuzungumza na mama au baba
yake.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:03


Next: Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.
Previous: Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions