Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.

      

Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.

  

Answers


Francis
Mwandishi amewapa wanawake nafasi mbili katika riwaya hii. Kuna nafasi ya juu/nafasi chanya – hurejelea namna mwandishi alivyomtukuza/alivyomjenga/alivyomuinua mwanamke, kwa mfano:

? Mwanamke ni mweledi. Tila alikuwa akimudu masuala ya sheria. Hakuna aliyempiku katika mijadala yaliyohusu masuala ya sheria.
? Wanawake ni wasomi. Umulkheri pia alisoma na kuhitimu vizuri.
? Mwanamke ni mwenye bidii. Tunaelezwa kuwa Umulkheri alikuwa nyuma yake Dick akiwa amepiga foleni. Anasafiri ng'ambo kwa shahada yake ya uhandisi katika masuala ya kilimo. Umu, baada ya kuchukuliwa na Mwangeka na Apondi alifanya bidii masomoni na kufuzu vyema katika mitihani yake.
? Mwanamke ni mwenye huruma - Apondi na Neema walijitwika jukumu la kuwalea wana ambao si wao kwa upendo na imani.
? Mwanamke ni jasiri - Zohali amewahi kupigana na majitu yaliyokuwa yakitaka kuuhujumu utu wake kwa kumnyanyasa kijinsia.
? Mwanamke ni mcheshi - Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza bali alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini.
Hali kadhalika, mwanamke amepewa nafasi ya chini/nafasi hasi. Hii hurejelea namna mwandishi alivyombomoa au alivyomuumbua au alivyomtweza mwanamke, kwa mfano:
? Mwanamke ni mjinga. Tuama alikuwa amejipata katika hali mbaya kwa kukubali kupashwa tohara. Alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake.
? Wanawake ni wahafidhina. Tuama anaitetea mila hii ya upashaji tohara kwa wanawake eti haijapitwa na wakati kwani bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto.
? Mwanamke ni katili na muuaji - Mamake Sauna anamsaidia Sauna kuavya mimba aliyokuwa amepachikwa na babake mlezi. Neema naye alikuwa ameavya mimba nyingi akiwa kwenye chuo kikuu.
? Mwanamke ni mwenye majuto - Neema alikuwa mwenye kujuta kwa kupoteza nafasi ya kupanga mtoto.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:06


Next: Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.
Previous: Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions