Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.

      

Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.

  

Answers


Francis
? Kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike aliyekuwa akisimuliwa katika visakale cha majirani zao na namna alivyowatumikisha wanaume kimetolewa kwa urejeshi.
? Ridhaa anakumbuka vijikaratasi vilivyoenezwa vikiwatahadharisha kuwa mna gharika baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya.
? Kisa cha namna Mzee Kedi (jirani yao) alivyomsaidia Ridhaa kupata shamba lake na kuwa ameyadhamini masomo ya wapwa zake wawili kimetolewa kwa urejeshi.
? Kisa cha yule mwana wa mlowezi maarufu aliyemiliki mashamba ya Theluji Nyeusi katika Eneo la Kisiwa bora kimetolewa kwa urejeshi.
? Mijadala baina ya Ridhaa na Tila imetolewa kwa njia ya urejeshi.
? Kaizari anasimulia yaliyojiri baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya aliyekuwa mwanamke kwa njia ya kurejelea.
? Mwangeka alipolitazama tabasamu la babake, alihisi kuwa sasa amezingirwa na uzio imara. Akawa anakumbuka wimbo ambao mamake alizoea kumwimbia kila mara babake alipokuwa ameenda katika safari za kikazi.
? Kisa cha namna Ami zake Kangata walivyokuwa wamekataa mwana wao aolewe na mtu wa ukoo mwingine kimetolewa kwa urejeshi.
? Moyo wa Kaizari ulipoanza kumsuta, alikumbuka kisa cha wafuasi wa Musa ambao baada ya kukosa chakula jangwani walimlaumu kwa kuwatoa kule Misri.
? Ridhaa alipokuwa ameketi kwenye chumba cha mapokezi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Rubia, alikumbuka namna walivyorudi nyumbani baada ya kuishi katika Msitu wa Mamba kwa miezi sita. Anakumbuka pia alivyokuwa akihisi.
? Ridhaa anakumbuka namna Tila bintiye alivyokuwa anapenda masuala yanayohusiana na sheria, haki na siasa.
? Kisa cha Lunga alivyostaafishwa kwa kuwa na msimamo imara kuhusiana na sakata ya mahindi kimetolewa kwa urejeshi.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:13


Next: Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.
Previous: “Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo) (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (b) Dondoo...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions