“Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo) (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (b) Dondoo...

      

“Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo)
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
(b) Dondoo hili linadokeza sifa gani ya mnenaji?
(c) Toa mifano miwili ya mbinu za lugha zilizotumika kifunguni.
(d) Linganisha mnenaji na mnenewa.

  

Answers


Francis
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
? Maneno haya yanasemwa na Majoka
? Anamweleza Tunu.
? Ni ofisini mwa Majoka.
? Tunu na Sudi wameenda kumwona. Majoka anadai yeye ni ami yake Tunu na anapoulizwa tangu lini akawa ami yake Tunu, anatoa maelezo haya.

(b) Dondoo hili linadokeza sifa gani ya mnenaji?
? Ni mwongo. Anadai kuwa na uhusiano wa karibu na babake Tunu.

(c) Toa mifano miwili ya mbinu za lugha zilizotumika kifunguni.
? Tashbihi – kulinganisha kwa kutumia viungo kama ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘kama’ na vinginevyo. Majoka anasema “...tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke...”
? Msemo - ndugu wa toka nitoke

(d) Linganisha mnenaji na mnenewa.
? Majoka ni kiongozi dhalimu ambaye anawanyanyasa wananchi ilhali Tunu ni kiongozi mwenye utu ambaye ndiye tumaini la Wanasagamoyo.
? Tunu ni msamehevu kwa vile anamsamehe Mamapima mwishoni mwa tamthilia, kinyume na Majoka ambaye ukimtenda basi hatokusamehe, atakudhuru. Amewaua wapinzani wake na wengine wakatiwa ndani.
? Tunu ni mwadilifu; licha ya tuhuma nyingi, hana uhusiano wa kizinifu na Sudi. Majoka ni mzinzi. Mkewe anadai hapatikani nyumbani na anatamani kuwa na uhusiano na Ashua ambaye ni mke wa mtu.
? Majoka anawakilisha wazee walio mamlakani ilhali Tunu anawakilisha vijana ambao wameamua kuwa viongozi ambao ndio tumaini la jamii.
? Tunu ni mtetezi wa wanyonge ilhali Majoka anawanyonga wanyonge.
? Tofauti ya kijinsia pia ambapo Tunu ni mwanamke ilhali Majoka ni mwanamume.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:16


Next: Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.
Previous: “Siafu huwa wengi. Si rahisi kuwamaliza.” (Kigogo) (a) Eleza muktadha wa nukuu. (b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu. (c) Eleza sifa tatu za mnenewa. (d) Kwa kifupi, fafanua...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions