(a) Eleza muktadha wa nukuu.
? Maneno haya yanasemwa na Hashima.
? Anamwambia Siti.
? Wako nyumbani kwake Hashima.
? Siti amekuja kumtembelea. Anamweleza kuhusu vijibarua vinavyosema jamii yake ihame lau sivyo watakomeshwa kama siafu.
(b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu.
? Sitiari – kufananisha vitu, watu au hali mbili bila moja kwa moja. Siafu ni sitiari ya kurejelea watu wanaodhulumiwa, katika muktadha huu jamii ya kina Siti.
(c) Eleza sifa tatu za mnenewa.
? Siti ni jasiri. Mlango wa nyuma wa nyumba ya Hashima unapobishwa, wote wanaingiwa na hofu, yaani Hashima, Tunu na Siti. Hata hivyo Siti anajipa ujasiri na kwenda kuchungulia ili amwone anayebisha.
? Ni msalihina. Anaamini Mungu atawaepushia tishio la kuangamizwa na utawala wa Majoka unaodai kuwa Sagamoyo si kwao. Anamwambia Tunu Mungu ni mwema. (uk. 54)
? Ni karimu. Anakubali wazo la Tunu la kuwachukua wanawe Sudi aende nao kuwapelekea Hashima awatunze hadi wazazi wao warejee.
? Ni mshauri mwema. Wakati Tunu anawaza kwa nini Sudi hajaenda kumtembelea na kuamini kuwa ni Sudi ndiye aliyemdhuru, Siti anamshauri asiwaze hivyo. Anamweleza kuwa anadanganywa ili asiweze kuwajua waliomdhuru. (uk. 54)
? Ana msimamo thabiti. Awali alikuwa mlevi na juhudi za Ngurumo kumshawishi kulewa tena zinagonga mwamba.
(d) Kwa kifupi, fafanua maudhui mawili yaliyodokezwa katika dondoo.
? Uhasama wa kikabila – unachangia kudhulumiwa kwa kundi moja na jingine lenye nguvu. Kabila la kina Kenga na Siti linatishwa kwa kuambiwa lihame eneo hilo kwa kuwa si kwao. Jamii hii isipofanya hivyo patakuwa na maafa; watakomeshwa kama siafu.
? Umoja – wanaodhulumiwa huwa wengi. Na wakiungana kama siafu hawawezi kuangamizwa kama Hashima anavyompa moyo Siti. Na hili linakuja kuwa kweli wakati Wanasagamoyo wanaungana na kuundoa utawala dhalimu wa Majoka mamlakani.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:20
- “Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo)
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
(b) Dondoo...(Solved)
“Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo)
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
(b) Dondoo hili linadokeza sifa gani ya mnenaji?
(c) Toa mifano miwili ya mbinu za lugha zilizotumika kifunguni.
(d) Linganisha mnenaji na mnenewa.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Fafanua namna mbinu ya kisengere nyuma ilivyotumika katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Fafanua nafasi ya mwanamke katika jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Mwanamke amedhalilishwa katika jamii. Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Eleza jinsi mapenzi yamejitokeza katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.(Solved)
Fafanua jinsi riwaya ya Chozi la Heri inavyosawiri elimu katika jamii.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Kwa kurejelea wahusika kadhaa, eleza jinsi mauti yameathiri jamii katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Fafanua jinsi ndoa inavyosawiriwa katika riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.(Solved)
Riwaya ya Chozi la Heri inadhihirisha jinsi migogoro inavyojitokeza katika jamii. Tambua migogoro hiyo.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
“Mabadiliko ni sehemu muhimu sana katika jamii.” Fafanua kauli hii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.(Solved)
Fafanua jinsi upotovu na uozo unavyodhihirika katika jamii ya riwaya ya Chozi la Heri.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa
tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea...(Solved)
“Nitajaribu, ila najua kwamba hili litanifanya kutengwa na wenzangu ambao kwa kweli ndio walionishikiza kupashwa
tohara. Sijui kama babangu atawahi kunisamehe kwa kumuasi.” “Atakusamehe. Mwana akinyea kiweo hakikatwi.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa dondoo.
(b) Tambua tamathali ya lugha iliyotumika katika dondoo.
(c) Ni maudhui yapi yanayojitokeza katika dondoo hili?
(d) Fafanua sifa mbili za mzungumzaji wa kauli ya kwanza.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali....(Solved)
“Nimechoka...nimechoka kuwatazama wagonjwa wakifa kwa kukosa huduma za kimsingi huku shehena za dawa zilizotengewa hospitali hii zikiishia kwenye maduka ya dawa ya wasimamizi wa hospitali. Nimechoka kuongolewa kwa wimbo wa performance contract.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa nukuu hii.
(b) Thibitisha tamathali mbili za usemi zinazodhihirika katika dondoo hili.
(c) Maudhui gani yanayowasilishwa katika dondoo hili?
(d) Kwa mujibu wa riwaya, ni mambo yapi yanayomchosha mzungumzaji wa kauli hii.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati. Bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Nisingepashwa tohara nisingeolewa. Msiba uliowapata wenzangu ni bahati mbaya tu.” (Chozi la...(Solved)
“Kupashwa tohara si mila iliyopitwa na wakati. Bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Nisingepashwa tohara nisingeolewa. Msiba uliowapata wenzangu ni bahati mbaya tu.” (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.
(c) Taja mbinu ya sanaa iliyotumika katika dondoo hili.
(d) Jadili hulka moja ya msemaji wa dondoo hili kwa kurejelea dondoo.
(e) Eleza kinyume cha kauli ya nafsineni kwa kurejelea hoja tano kutoka kwenye riwaya.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri)
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu.
(b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama...(Solved)
“Hii ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mungu amenifidia yule mwanangu aliyekufa.” (Chozi la Heri)
(a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake faafu.
(b) Taja ‘baraka’ zilizomwandama msemaji maishani.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa...(Solved)
“Suala la polisi na wanajeshi kutatua mizozo midogomidogo kwa makeke na bunduki ni jambo ambalo limeanza kupitwa na wakati; ni sawa na kumuua chawa kwa fimbo!”
(a) Weka maneno haya katika muktadha wake.
(b) Fafanua masuala mengine saba aliyowasilisha mzungumzaji.
(c) Kwa kurejelea sehemu nyinginezo za riwaya, jadili sifa zozote nne za mzungumzaji wa dondoo hili.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa...(Solved)
“Baba amekonga zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge...sasa amemshamiri Babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.” (Chozi la Heri)
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza masaibu yaliyomkumba baba anayerejelewa maishani mwake.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- “Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii.
(c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji...(Solved)
“Kumbe hata wewe shemeji...upo? (Chozi la Heri)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza sifa zozote tatu za msemaji wa kauli hii.
(c) Taja changamoto walizopitia mzungumzaji na wakimbizi wengine katika kambi ya wakimbizi.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.(Solved)
Mabadiliko ni maudhui yaliyojadiliwa kwa kina na mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)
- Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.(Solved)
Riwaya Chozi la Heri imeathiriwa pakubwa na tanzu za fasihi simulizi. Jadili.
Date posted: February 6, 2023. Answers (1)