Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Siafu huwa wengi. Si rahisi kuwamaliza.” (Kigogo) (a) Eleza muktadha wa nukuu. (b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu. (c) Eleza sifa tatu za mnenewa. (d) Kwa kifupi, fafanua...

      

“Siafu huwa wengi. Si rahisi kuwamaliza.” (Kigogo)
(a) Eleza muktadha wa nukuu.
(b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu.
(c) Eleza sifa tatu za mnenewa.
(d) Kwa kifupi, fafanua maudhui mawili yaliyodokezwa katika dondoo.

  

Answers


Francis
(a) Eleza muktadha wa nukuu.
? Maneno haya yanasemwa na Hashima.
? Anamwambia Siti.
? Wako nyumbani kwake Hashima.
? Siti amekuja kumtembelea. Anamweleza kuhusu vijibarua vinavyosema jamii yake ihame lau sivyo watakomeshwa kama siafu.

(b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu.
? Sitiari – kufananisha vitu, watu au hali mbili bila moja kwa moja. Siafu ni sitiari ya kurejelea watu wanaodhulumiwa, katika muktadha huu jamii ya kina Siti.

(c) Eleza sifa tatu za mnenewa.
? Siti ni jasiri. Mlango wa nyuma wa nyumba ya Hashima unapobishwa, wote wanaingiwa na hofu, yaani Hashima, Tunu na Siti. Hata hivyo Siti anajipa ujasiri na kwenda kuchungulia ili amwone anayebisha.
? Ni msalihina. Anaamini Mungu atawaepushia tishio la kuangamizwa na utawala wa Majoka unaodai kuwa Sagamoyo si kwao. Anamwambia Tunu Mungu ni mwema. (uk. 54)
? Ni karimu. Anakubali wazo la Tunu la kuwachukua wanawe Sudi aende nao kuwapelekea Hashima awatunze hadi wazazi wao warejee.
? Ni mshauri mwema. Wakati Tunu anawaza kwa nini Sudi hajaenda kumtembelea na kuamini kuwa ni Sudi ndiye aliyemdhuru, Siti anamshauri asiwaze hivyo. Anamweleza kuwa anadanganywa ili asiweze kuwajua waliomdhuru. (uk. 54)
? Ana msimamo thabiti. Awali alikuwa mlevi na juhudi za Ngurumo kumshawishi kulewa tena zinagonga mwamba.

(d) Kwa kifupi, fafanua maudhui mawili yaliyodokezwa katika dondoo.
? Uhasama wa kikabila – unachangia kudhulumiwa kwa kundi moja na jingine lenye nguvu. Kabila la kina Kenga na Siti linatishwa kwa kuambiwa lihame eneo hilo kwa kuwa si kwao. Jamii hii isipofanya hivyo patakuwa na maafa; watakomeshwa kama siafu.
? Umoja – wanaodhulumiwa huwa wengi. Na wakiungana kama siafu hawawezi kuangamizwa kama Hashima anavyompa moyo Siti. Na hili linakuja kuwa kweli wakati Wanasagamoyo wanaungana na kuundoa utawala dhalimu wa Majoka mamlakani.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:20


Next: “Mimi na marehemu babako... wajua tulikuwa kama ndugu wa toka nitoke japo hatuna uhusiano wa damu.” (Kigogo) (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (b) Dondoo...
Previous: “Mmetamauka nyinyi. Wewe na huyu mpenzi wako Sudi mmetamauka. Sagamoyo ni pazuri zaidi tangu soko lilipofungwa.” (Kigogo) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza sifa tatu...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions