Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“Mmetamauka nyinyi. Wewe na huyu mpenzi wako Sudi mmetamauka. Sagamoyo ni pazuri zaidi tangu soko lilipofungwa.” (Kigogo) (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (b) Eleza sifa tatu...

      

“Mmetamauka nyinyi. Wewe na huyu mpenzi wako Sudi mmetamauka. Sagamoyo ni pazuri zaidi tangu soko lilipofungwa.” (Kigogo)
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza sifa tatu za msemaji.
(c) Fafanua umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
(d) Eleza jinsi mbinu ya kinaya ilivyotumiwa katika dondoo hili.

  

Answers


Francis
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
? Maneno haya yanasemwa na Ngurumo.
? Anamwambia Tunu.
? Tunu na Sudi wamefika Mangweni kukutana na waliomdhuru Tunu.
? Ngurumo anayasema maneno haya baada ya Tunu kumuuliza ni lipi lenye umuhimu kati ya kufunguliwa kwa soko na kuhudhuria dhifa iliyoandaliwa na kigogo.

(b) Eleza sifa tatu za msemaji.
? Ngurumo ni mpenda anasa. Anajulikana sana Sagamoyo kwa uraibu wake wa vileo.
? Ngurumo ni mzinzi. Asiya alipata mradi wa keki kwa kumpa Ngurumo uroda.
? Ni mwenye kejeli. Anatumia kejeli anapowazungumzia Sudi na Tunu. Anakejeli uhusiano wa Tunu na Sudi.
? Ni mwenye mtazamo finyu kuhusu maisha. Haoni faida ya kufunguliwa kwa soko la Chapakazi. Anaona heri kuhudhuria sherehe za uhuru.

(c) Fafanua umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
? Tunu anawakilikisha tapo la wananchi waliochoshwa na udhalimu wa viongozi wa kisiasa na wakaamua kuongoza harakati za ukombozi.
? Mwandishi amemtumia kufanikisha dhamira yake kwa kuonyesha nguvu walizonazo wanawake katika kuleta mabadiliko katika jamii. Anaongoza umma kupinga na kuuondoa utawala dhalimu wa Majoka.
? Mwandishi amemtumia Tunu kuondoa dhana kuwa wanawake ni viumbe dhaifu. Wanaweza kushiriki vilivyo kuleta mabadiliko kwenye jamii; bega kwa bega na wanaume.
? Ametumiwa kujenga sifa za wahusika wengine kama Majoka, Sudi na Ngurumo.
? Ametumiwa kufanikisha matumizi ya mbinu mbalimbali za sanaa katika tamthilia.

(d) Eleza jinsi mbinu ya kinaya ilivyotumiwa katika dondoo hili.
? Ni kinaya Ngurumo kusema kuwa Sagamoyo ni pazuri zaidi tangu soko lilipofungwa ilhali wanasagamoyo wamekosa mahali pa kupata riziki yao.
? Ni kinaya Ngurumo kudai kuwa Tunu na Sudi wametamauka ilhali wana tamaa ya kuona mabadiliko ya kweli yamesheheni Sagamoyo.
? Ni kinaya kwa Ngurumo kudai kuwa Sudi ni mpenziwe Tunu ilhali si mpenziwe. Ni kinaya pia kuwashuku Tunu na Sudi kuwa na uhusiano wa uzinifu ilhali yeye na Asiya wamekuwa na uhusiano kama huo.
? Inatarajiwa Ngurumo awe anajiunga na Wanasagamoyo wengine kupigania kufunguliwa kwa soko ili wananchi wapate mahali pa kupata riziki badala yake analiona hilo kuwa halina maana.
francis1897 answered the question on February 6, 2023 at 07:23


Next: “Siafu huwa wengi. Si rahisi kuwamaliza.” (Kigogo) (a) Eleza muktadha wa nukuu. (b) Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika humu. (c) Eleza sifa tatu za mnenewa. (d) Kwa kifupi, fafanua...
Previous: Bainisha matatizo ambayo Wanasagamoyo wanakumbana nayo katika upiganiaji wa haki katika eneo la Sagamoyo katika tamdhilia ya Sagamoyo.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions